WAFANYABIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA WACHINJANA KAMA KUKU MEXICO...

KUSHOTO: Tajiri Miguel Angel Trevino Morales. JUU: Wafuasi wa kundi la Zetas wakiwa wamekamatwa. CHINI: Wafuasi wa kundi la Gulf wakiwa wamepangwa mstari kabla ya kuchinjwa kama walivyonaswa kwenye video.
Video ya kutisha inayoonesha wafuasi wa kundi la dawa za kulevya la Mexico wakikatwa vichwa na kundi la wapinzani wao imesambazwa kwenye mtandao wa intaneti katika uovu wa hivi karibuni katika mapambano dhidi ya biashara ya dawa hizo.
Video hiyo ambayo imesambazwa kwenye blog ya Mundonarco.com inayomilikiwa na muungano wa kudhibiti biashara hiyo, inaonesha wafuasi waliofichwa sura zao wa Kundi la Gulf wakiwa wamesimama nyuma ya wafuasi wa Zetas waliokuwa vifua wazi ambao wamechorwa alama nyeusi ya 'Zs' kwenye vifua vyao.
Wanaume waliofichwa sura walikuwa wameshikilia mapanga na kuwazaba vibao wafungwa wao, ambao wanapiga magoti chini mbele yao huku kila mmoja akijitambulisha jina lake kwenye kamera.
Walipoulizwa nani kawatuma, kila mmoja alijibu 'Z-40'.
40 ni jina alilopewa Miguel Angel Trevino Morales, kiongozi wa pili kwa ukubwa katika kundi la Zeta.
Mtu aliyepiga picha hizo za video aliwaambia: "Mmejikuta hapa sababu mlikuja kutufanya vibaya. Kaa tayari, wanaume."
Kisha kamera inawaonesha wanaume watatu kati yao wakianza taratibu kuwakabili huku wakiwakatakata shingo zao kwa mapanga.
Huku watu hao wakipiga kelele za kuomba msamaha, mpigapicha za video hiyo alisema: "Hivi ndivyo watu wenu wote wachafu mtakavyoishia."
Baada ya zoezi hilo kukamilika, baada ya takribani dakika mbili za kupokea maumivu makali, watu walioficha sura zao walinyanyua juu vichwa kadhaa kama vikombe vyao vya ubingwa.
Majaliwa ya watu watatu tu kati ya watano yameoneshwa bayana.
Mundonarco.com imeeleza video hiyo ilirekodiwa kwenye mjini Rio Bravo, Mexico kando ya mpaka wa Marekani.
Kundi la Zetas lilianzishwa na askari wa zamani waliojiengua kwenye jeshi la Mexico mwaka 1998 kufanya kazi kama wauaji wa kukodiwa kwa ajili ya wasafirishaji wa dawa za kulevya.
Tangu wakati huo wamejenga himaya yao ya biashara ya dawa za kulevya, ikipanuka kwa kasi kubwa katika Mexico yote na kujiingiza katika utekaji nyara, uporaji wa kutumia nguvu na wizi wa mafuta ghafi.
Juni 10, mwaka huu miili iliyokatwa viungo ya wanaume 11 na wanawake watatu ilikutwa katika mji maarufu kwa kilimo cha miwa wa Ciudad Mante uliopo Kusini mwa Jimbo la Tamaulipas ambao unapakana na Texas.
Tamaulipas umekuwa mmoja wa miji iliyoshamiri kwa mapambano makali ya umwagaji damu katika vita ya dawa za kulevya nchini Mexico.
Siku tano tu kabla, Polisi wa Mexico walikuta miili saba iliyokatwa viungo kwenye jimbo la pwani ya Pacific la Sinaloa, sambamba na ujumbe ukishutumu mamlaka husika kushirikiana na Tajiri wa dawa hizo, Joaquin 'El Chapo' Guzman, mtu anayesakwa kwa udi na uvumba nchini humo.
Miili hiyo ilikuwa imepangwa kwenye magunia 13 meusi mapema Juni 5 na kutupwa kwenye njia ya watembea kwa miguu katika eneo la makazi ya watu, mamlaka zimesema.
Guzman, ambaye kwa kipindi kirefu ametambulika kama kigogo wa dawa za kulevya mwenye nguvu zaidi Mexico, alihusishwa mwaka huu katika orodha ya Forbes ya watu matajiri zaidi duniani, akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia Dola za Marekani bilioni 1.
Alitoroka gereza la Mexico mwaka 2001 kwa kutumia lori la usafi akiwa kajitwisha Dola za Marekani milioni 7 kichwani mwake.
Januari, Los Zetas lilisambazwa video ikionesha kunyongwa wafuasi wawili wa kundi la Gulf na mwezi uliopita miili 49 iliyochinjwa ikiwa imetupwa kando ya barabara kuu kutoka kundi hilo hilo.
Serikali ya Marekani imetoa ofa ya Dola za Marekani milioni 5 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa 40.
Kwa ujumla, karibu watu 55,000 wamekufa katika matukio yanayohusiana na vurugu za dawa za kulevya na zaidi ya 5,000 hawajulikani waliko nchini Mexico tangu Rais Felipe Calderon alipoingia madarakani Desemba mwaka 2006.
Wiki iliyopita, Ikulu ilitahadharisha wasafiri wa Marekani kwenye Mexico kuchukua tahadhari ya kuwako mashambulio ya kulipa kisasi kufuatia kukamatwa kwa wanaodaiwa kuwa washirika wa kundi la dawa za kulevya la Zetas ndani ya Marekani.

No comments: