WAFA BAADA YA KUGONGANA NA KULALIWA NA LORI...

Mwanaume na mwanamke wamefariki baada ya gari lao kugongana, kisha kulaliwa na lori katika ajali iliyotokea kwenye barabara kuu.
Ajali hiyo ya kutisha ililazimisha kufungwa kwa barabara wa magari ya mizigo kwenye makutano namba 26 mjini Cleckheaton huko West Yorkshire ambapo lori aina ya Mercedes lilipogongana na gari dogo aina ya Audi A5.
Watu waliokuwamo kwenye Audi, mwanaume mwenye miaka 46 na mwanamke mwenye miaka 43, wanaodhaniwa kuishi Bishop Auckland, mjini Durham, walikufa papo hapo baada ya lori kupinduka na kulalia gari dogo karibu nusu ya gari.
Kufungwa kwa barabara, ambayo sasa imefikia zaidi ya masaa 10, inasababisha msongamano mkubwa wa magari huko katika maeneo ya Birkenshaw, Liversedge, Heckmondwike, Mirfield na Ravensthorpe.
Msemaji wa polisi alisema kwamba ufungwaji huo wa barabara ulitarajiwa kuendelea hadi baadaye jana wakati uchunguzi ukiendelea kutafuta sababu ya ajali hiyo.
Wakati polisi wakiwa hawajui jinsi ajali hiyo ilivyotokea, mikwaruzo na alama za maguduru ya magari hayo zinaashiria ajali imechangiwa na mwendokasi uliosababisha ajali hiyo mbaya.
Dereva wa lori mwenye miaka 43 anayetokea North East Lincolnshire, mjini Yorkshire alikimbizwa hopsitali kutokana na majeraha madogo aliyopata.
Timu ya Uchunguzi wa Ajali (MCET) imeomba mashuhuda kuchangia kutoa taarifa zitakazosaidia uchunguzi.
Sajenti Garry Alderson wa MCET alisema: "Ni wazi hii ilikuwa ajali mbaya sana ambayo imesababisha vifo vya mwanaume na mwanamke waliokuwa wakisafiri kwa gari lao aina ya Audi.
"Tutafanya uchunguzi kamili wa kugongana kwenye eneo la tukio na kwamba hii itachukua muda ili kulipa uzito tukio lenyewe.
"Ningewashauri madereva kukwepa eneo hili ikiwezekana wakati kazi ya kuyaondoa magari yaliyohusika ikikaribia kuanza na kumtaka yeyote aliyeshuhudia ajali hiyo kuwasiliana na timu yetu."

No comments: