SARATANI YA MATITI YAKATISHA UHAI WA MKALI WA FILAMU ZA NGONO...


KUSHOTO: Hollie Stevens. KULIA: Hollie akiwa na mumewe, Eric Cash.
 Nyota wa filamu za watu wazima anayefahamika kama 'Queen of Clown Porn' amefariki baada ya kupambana na maradhi ya saratani ya matiti akiwa na umri wa miaka 30 tu.
Hollie Stevens anayeishi San Fransisco, mjini Clifornia, alifariki huku akiwa kashikilia mkono wa mumewe hospitalini Jumanne iliyopita baada ya saratani kusambaa kwenye mifupa yake, ini na ubongo.
Hollie, ambaye aliolewa mwezi uliopita tu, amecheza zaidi ya filamu 170 na kuchaguliwa kwa tuzo kadhaa katika tasniya hiyo. Alikuwa pia mfuasi wa niche genre, filamu za ngono za vichekesho.
Lakini kabla ya kifo chake, alisema alitumaini kukumbukwa kama mke mwema na rafiki badala ya majukumu yake ya kitaaluma.
"Natumaini watu wanaelewa kwamba siku nzote nimekuwa mwenyewe. Nasikia fahari katika kile wengine wanachofikiri kinaweza kuwa miujiza kuhusu mimi!" alisema.
"Ninataka pia watu kujua ninachopendelea zaidi, kile kinachonipa furaha, ni kuwa rafiki na pia mke. Hicho ndicho ninataka wajue na kukumbuka."
Aligundulika kuwa na Hatua ya Tatu ya Saratani ya matiti mwaka jana na baadaye akafanyiwa upasuaji kwa miezi kadhaa, ambapo alikatwa titi lake la kushoto.
Taarifa baada ya uchunguzi wa mwili wake ulibaini kwamba kulikuwa na uvimbe ndani ya titi lake lakini akapuuzia matibabu kutokana na kutokuwa na bima ya afya.
"Niligundua na kuchukua tahadhari kubwa, lakini kwenda kumwona daktari ni vigumu pale unapokuwa huna bima," aliwahi kusema.
Rafiki zake, familia na mashabiki walisaidia kumchangia Dola za Marekani 16,000 kwa ajili ya kulipa gharama zake za matibabu.
"Siamini watu wangapi wanaojali, jinsi mashabiki wangu walivyo wakarimu, na kiasi gani watu wageni kabisa kwangu walivyonisaidia," alisema akizungumzia michango. Si kila mtu anachukia clowns!"
Kati ya wote walioongoza kampeni ya kumchangia alikuwa January Seraph, ambaye aliwataka wateja wake kuchangia fedha katika muda wa ziada wa kazi yake.
Kupitia moja ya blogu zake ya 'missjanuary.com', Seraph aliahidi kutoa nyongeza ya nusu saa katika muda wake wa kawaida kwa mteja yeyote ambaye angechangia Dola za Marekani 50 kwa Mfuko wa Matibabu ya Hollie Stevens.
July 2011, alisema alikuwa akihamasisha watu kumsaidia Hollie apone sababu rafiki yake hawezi kufanya hivyo.
Alisema: "Alisikia fahari kuomba msaada mwenyewe, hivyo mimi na marafiki zake wengine wakubwa tumesukumwa na kumsaidia apende au asipende.
"Kuonesha jinsi Hollie anavyopendwa na kukubalika katika kipindi chake. Sababu hakuna atakayejisikia mpweke siku atakapokuwa mgonjwa."
Lakini Desemba 2011, saratani iligundulika kusambaa kwenye mifupa yake.
Machi, uvimbe mdogo uligundulika kwenye mguu wa mwigizaji huyo na akafanyiwa upasuaji kujaribu kuimarisha mguu na paja lake.
Mizizi ya saratani ilikutwa pia kwenye ini lake na sehemu mbalimbali ambako ilionekana kuwa katika hatua za awali.
Alishindwa mapambano hayo Jumanne ya Julai 3 mjini San Fransisco huku akiwa ameshikilia mkono wa mumewe, mchekeshaji na mwigizaji Eric Cash, ambaye alifunga naye ndoa hospitalini Juni.
Amekuwa akiingiza mashabiki wapya kwenye mtandao wa Twitter kila mara sambamba na picha zilizopigwa nje ya hospitali, ambazo alionekana mwenye nuru na tabasamu pana.
Picha nyingine zilimuonesha akiwa amewekewa dripu na kuongezewa damu, wakati meseji nyingine zilisema jinsi gani alivyo na hamu ya kumuona mume wake mpya.
Licha ya kufanya kazi kama nyota wa picha za ngono, mchekeshaji na mwigizaji, Hollie pia alifurahia kuchora na kuoneshakazi zake kwenye Maktaba ya Hyena iliyoko mjini Burbank, imeelezwa.

No comments: