RAPA FRANK OCEAN WA ODD FUTURE AJITANGAZA KUWA SHOGA...

Mshirika wa Kanye West, Frank Ocean anayetokea katika kundi la rap la Odd Future ameweka hadharani kuwa ni shoga au mtu mwenye mahusiano ya jinsia moja.
Kukiri huko kunamfanya Ocean kuwa nyota wa kwanza wa hip hop kuweka hadharani na hivyo kuanza kuwavutia wanaume.
Ocean, ambaye aliwashirikisha Kanye na Jay-Z katika "Watch the Throne", ametuma ujumbe mrefu wa kina hivi karibuni akiandika, "Miaka minne iliyopita, nilikutana na mtu fulani. Nilikuwa na miaka 19. Na yeye pia."
"Tulitanua wakati huo, na baada ya hapo, pamoja. Karibu kila siku. Na siku zilizofuatia tulikuwa pamoja, muda ulisonga kasi. Siku nzima nilimuona, na tabasamu lake."
"Nililala naye. Wakati nilipobaini nimezama kwenye mapenzi, nilikuwa hoi taabani. Sikuwa na jinsi. Hakukuwa na pa kutokea, sikuweza kuwasiliana na wanawake wangu niliokuwa nao, wale niliokuwa nikiwajali na kudhani walikuwa wapenzi wangu."
Aliongeza, "Sina siri zozote ninazohitaji kuficha zaidi… Najihisi kama mtu huru."
Kumekuwa hakuna kabisa uvumilivu katika dunia ya hip hop kuhusiana na ushoga na mahusiano ya jinsia moja, hivyo kujiweka wazi kwa Frank kumeibua uwazi. Itafungua milango kwa nyota wengine ambao walikuwa wakifikiria kufanya hivyo kujitokeza.
Msanii mwenzake we Bendi ay Odd Future, Tyler the Creator ametuma ujumbe baada ya Frank kutuma, akiandika, "Hatimaye kaka yangu amefanya hivyo. Ni faraja kubwa sababu najua kufanya hivyo ni Ngumu au Vinginevyo."

No comments: