Mbunge wa Mwibara, ambaye ni polisi mstaafu, Kangi Lugola (CCM), ametoa shutuma nzito bungeni akisema kuna mtandao mkubwa wa uhalifu unaohusisha askari Polisi huku akimtaja kwa jina, akisema ndiye kinara.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo amesema daima Polisi itaendelea kuwa nyuma ya wahalifu na ni ndoto kukabiliana na majambazi kwa vile inatumia mbinu na zana dhaifu ikilinganishwa na teknolojia na umahiri wa mbinu za majambazi.
Alisema hayo bungeni mjini hapa jana alipochangia hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kuhusu mapato, makadirio na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13.
Huku akimtaja Fadhil Kweka, kuwa askari anayeongoza mtandao huo huku akiahidi kutoa ushahidi. Hata hivyo, hakuna mbunge aliyesimama kuomba Mwongozo wa Spika kutokana na Lugola kumtaja Kweka ambaye hana nafasi ya kujitetea.
Lugola alisema ni lazima Serikali ikomeshe mtandao huo wa askari wanaojihusisha na uhalifu mara moja vinginevyo ni ndoto kwa uhalifu kumalizika.
Alisema mbinu zinazotumiwa na Polisi katika kukabiliana na majambazi ni za kizamani zinazotokana na ukosefu wa zana za kisasa na wakati majambazi wakitumia vifaa vya kisasa, polisi wanajivunia virungu na filimbi.
"Hizi ni ndoto, ni lazima polisi sasa wapewe kamera, wawe na vifaa vya DNA (utambuzi wa vinasaba), na fedha za kutosha za kuliwezesha Jeshi hilo kununua taarifa za siri kuhusu mipango ya uhalifu maana taarifa hizi sasa zinauzwa kwa gharama kubwa sana," alisema Lugola.
Alisema anashangazwa na hatua ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuendelea kupungua mwaka hadi mwaka, hatua ambayo alisema inatumiwa kama mwanya kwa wahalifu ambao alisema sasa ni wadau wakubwa wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani na wamekuwa wanaifuatilia ili kujua namna Serikali inavyoelekeza nguvu zake katika kukabiliana na uhalifu.
"Hili ni jambo la ajabu sana. Mwaka 2010, Serikali ilitenga asilimia 71 ya fedha kwa Wizara hii, mwaka 2011 ikatenga asilimia 79 ya fedha zote na sasa imetenga asilimia 74, hii ni ishara wazi kwamba Jeshi la Polisi litaendelea kuwa nyuma ya wahalifu," alisema Lugola.
Alishangazwa na hatua ya Serikali kushindwa kutoka Sh 225,000 za posho kwa Polisi kama inavyofanya kwa askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na kupanga kutoa Sh 150,000 alizosema zinawafanya askari kutokuwa na afya njema na kupata vitambi visivyo na mpangilio na majambazi kuwanyang’anya silaha kirahisi kutokana na kukosa lishe bora.
Mapema akiwasilisha hotuba hiyo, Dk Nchimbi alisema idadi ya makosa ya jinai imeongezeka kwa asilimia 3.9, kwa mwaka uliopita kutokana na mmomonyoko wa maadili, tamaa ya utajiri wa haraka haraka, imani za kishirikina, tamaa ya maisha na umasikini, lakini Jeshi la Polisi limeendelea kubuni na kutekeleza mikakati ya aina mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu nchini ukiwamo Mkakati wa Ulinzi Shirikishi.
Alisema pia limekuwapo ongezeko la ajali za barabarani zinazoangamiza wananchi wengi kwa kuwapotezea maisha na kuwasababishia ulemavu wa kudumu.
Alisema hatua mbalimbali zinachukuliwa kama kutoa elimu, kuhuisha adhabu, kushirikisha wadau, kuendeleza doria, kufanya ukaguzi, kutumia kamera na kusimamia utoaji wa leseni mpya za magari.
Aliongeza pia kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kuchukua hatua za kuhakikisha nchi inakuwa na usalama, amani na utulivu kwa kudhibiti silaha za kiraia, kutumia jukwaa la Haki Jinai, kushirikiana na polisi kikanda na kimataifa na kuboresha maslahi ya askari, kutoa ajira na kujenga vituo vya Polisi.

No comments:
Post a Comment