Eneo la Ogbadibo, nchini Nigeria ambako tukio hilo limetokea.
Mfanyabiashara maarufu na mume wa wake sita, amefariki baada ya kudaiwa kuwa alilazimishwa kufanya mapenzi na mfululizo na wake zake wote sita 'wenye wivu'.Mnigeria Uroko Onoja alifanya mapenzi na mke wake mdogo huku wengine watano waliobaki inasemekana walikuwa wamemuelekezea visu na fimbo na kumtaka akimaliza hapo afanye mapenzi na kila mmoja wao.
Onoja alimudu kufanya hivyo na wake zake wanne mfululizo, lakini 'akaacha kupumua' wakati mke wa tano akijiandaa kupanda kitandani kwenye nyumba yao iliyoko Ogbadibo, kwa mujibu wa gazeti la Daily Post la Nigeria.
Wanawake wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo lililotokea katika jimbo la Benue wiki iliyopita, zilisema ripoti, ambazo zimetumia neno "kubakwa hadi kufa" zikielezea mkasa uliomkumba mfanyabiashara huyo.
Imeelezwa Onoja alikuwa amerejea kutoka baa kwenye eneo la jamii ndogo ya Ugbugbu, Ogbadibo, majira ya saa 9 alfajiri Jumanne, na kuelekea kitandani alikolala mke wake mdogo.
Wake sake winging watano, ambao inasemekena walikuwa na kikao kujadili mpango wao kabla ya mume wao kurejea nyumbani, wakati huo wanadaiwa kuvamia chumbani humo wakiwa na visu na fimbo kushinikiza kupewa haki yao ya unyumba.
Mfanyabiashara huyo, ameelezewa kama mfadhili ambaye 'amechangia mafanikio' katika ukuaji wa jamii yake ndogo, anadhaniwa kukaidi matakwa hayo ya wake zake kabla ya kuzidiwa nguvu.
Onoja inasemekana alishindwa kupumua na kushindwa kurudisha fahamu baada ya kufanya mapenzi na wake zake wanne mfululizo.
Mke wake mdogo alinukuliwa kusema wake wenzake watano walikimbilia msituni baada ya kugundua kwamba mume wao amefariki.
Mkuu wa Kijiji, Okpe Odoh, ameliambia Daily Post tukio hilo tayari limeripotiwa polisi.
No comments:
Post a Comment