Wasafiri wa mara kwa mara wanafahamu vyema jinsi ugumu wa ukaguzi kwenye Uwanja wa Ndege unavyoweza kuwa.
Liam Corcoran mwenye miaka 11, alimtoroka mama yake, akapanda basi hadi Uwanja wa ndege ulioko maili tatu kutoka hapo na kupanda ndege kuelekea mjini Roma bila mtu yeyote kumhoji kwa hicho alichokuwa akifanya.
Ni pale tu alipoanza kutamba kwamba ametoroka nyumbani wakati ndege ilipokuwa ikipita Ufaransa ndipo abiria wengine wakawataarifu wafanyakazi wa kwenye ndege.
Pamoja na kusababisha masaa kadhaa ya hofu na mashaka kwa mama wa Liam, Mary mwenye miaka 29, uvunjikaji wa kushangaza wa ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Manchester muda mfupi kabla ya kuanza Michezo ya Olimpiki imeibua maswali mengi kuhusu ulinzi wa mipaka ya Uingereza.
Juzi baba wa Liam, Aaron Fort mwenye miaka 34, aliongelea kukosa kwake imani kwamba hakuna yeyote uwanjani hapo aliyehoji alichokuwa akifanya pale mtoto huyo asiye na mwangalizi.
Alibainisha kwamba Liam, ambaye alishawahi kutoroka siku za nyuma, kuwa hajawahi kupanda ndege kabla na wala hana pasi ya kusafiria.
Fort alisema: "Liam alinieleza kwa mara ya kwanza anajua yuko katika matatizo pale tu ndege ilipoanza kuruka na kuacha ardhi. Alifanya vitu tofauti na maelekezo ya wahudumu na alikaa kwenye kiti chake huku akiwa kajifunga mkanda."
Punde abiria wengine walipotoa taarifa, wahudumu wa ndege wakawataarifu wenzao walioko uwanjani kuhusu mzamiaji huyo.
Walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Fiumicino mjini Roma, Liam aliachwa ndani ya ndege wakati ndege hiyo ikifanyiwa maandalizi kwa safari ya kurudi. Mwishowe, masaa nane baada ya kuruka kutoka Manchester, akaungana na mama yake aliyepata amani baada ya kuishi kwa mashaka makubwa.
Wakati Maofisa usalama wa Uwanja wa Ndege wakikuwa katika tahadhari kubwa kipindi kwa hofu ya kutokea shambulio la ugaidi wakati wa Michezo ya Olimpiki, Waziri wa Uchukuzi Justine Greening alisema: "Nachukulia udhaifu wa usalama kwa umakini mkubwa sana, hivyo sasa tunapitia kwa haraka na Uwanja wa Manchester, na ndege husika, kujua hasa nini kilichotokea."
Wakati huohuo, Shirika la Ndege la Jet2 lilisema limewasimamisha wafanyakazi wake watatu ambao walimruhusu Liam kuingia na sasa wamekuwa wakihesabu abiria kwenye ndege zake zote.
Baba wa Liam ameeleza kwamba mtoto wake alikuwa akiogolea na mama yake huko Wythenshawe, mjini Manchester, ndipo mkasa huo ulipoanza Jumanne iliyopita.
Fort, ambaye alitengana na mama wa Liam na sasa anaishi mjini Blackpool, alisema mtoto wake alilazimika kulindwa na mlinzi.
"Mfululizo wa tukio zima unaweza kuwa umemwogopesha," aliongezea mfanyakazi mmoja wa duka. "Amekuwa na matatizo katika kusoma na kutojichanganya na watoto wengine. Lazima atakuwa amebadilika na kumtoroka mama yake."
Baada ya safari yake kwa basi, Liam akaingia Terminal 1 majira ya Saa 7 mchana na kujichanganya na familia ambayo ilikuwa ikijiandaa kwenda kukaguliwa na watu wa usalama.
Chanzo kimoja cha habari uwanjani hapo kilisema: "Hutokea mzazi mmoja akawa na pasi za kusafiria kwa ajili ya watoto wake wote, hivyo walinzi wa usalama wanatakiwa kuhesabu pasi hizo na watoto husika, lakini ni wazi kwamba walishindwa kugundua kuwa kuna mmoja amezidi."
Alieleza kwamba Liam alipita kwenye mashine ambazo zingeweza kubaini kama amebeba kitu chochote cha hatari.
Baada ya kumaliza taratibu za safari, alielekea kwenye geti la kwanza aliloliona. Akadhaniwa tena kwamba ameambatana na familia fulani, na mfanyakazi wa Jet2 alishindwa kutambua hakuwa na nyaraka zozote wakati akikaa kwenye kiti cha ndege.
Abiria mmoja kwenye ndege hiyo wakati wa kurudi, Sarah Swayne mwenye miaka 26 kutoka Nantwich alisema: "Alikuwa muongeaji sana na kuonekana asiyesumbuka kwa hilo hata kidogo."
Mama wa Liam hakuwapo nyumbani kwake katika maghorofa ya Newall Green hiyo juzi, lakini majirani walisema: "Nadhani atakuwa shujaa kwa kiasi fulani mbele ya marafiki zake kwa kufanikisha hilo."
Ndugu yake mmoja aliongeza: "Liam mwenye kupenda kusikilizwa, amekuwa akitoroka mara kwa mara. Lakini hakuwahi kufanya kitu kama hiki. Katili huyu mdogo aliruka hadi mjini Roma."
Msemaji wa Uwanja wa Ndege wa manchester alisema uzembe huo unafanyiwa 'uchunguzi wa haraka', lakini akaongeza: "Mtoto huyo alikaguliwa kikamilifu hivyo usalama wa abiria haukuwa katika mashaka yoyote."

No comments:
Post a Comment