Ajali mbaya ya meli imeikumba Tanzania tena ambapo zaidi ya watu 20 wamethibitika kufariki dunia na wengine hawajulikani walipo baada ya meli aina ya Mv Skagit inayomilikiwa na Kampuni Seagul Transport, kuzama karibu na kisiwa cha Chumbe, Kilometa za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) zilizotumwa jana kwa vyombo vya habari, meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 300, iliondoka Bandari ya Dar es Salaam jana saa 06.05 mchana ikiwa na abiria 248, watoto 31 na mabaharia 9.
Taarifa hiyo iliyotumwa na Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray, ilieleza kuwa meli hiyo iliyosajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), cheti chake cha ubora kilichoanza Agosti 24 mwaka jana, kilikuwa kinamalizika muda wake Agosti 23, mwaka huu.
Meli hiyo imezama siku chache kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza kati ya Ijumaa au Jumamosi, ambapo wananchi wengi wa Zanzibar husafiri kwenda kisiwani huko.
Hii ni ajali ya pili kutokea takriban mwaka mmoja sasa nyingine ikiwa ni ya Septemba mwaka jana, ambapo meli ya Mv Spice Islander ilizama katika eneo la Nungwi na kuua watu wasiopungua 187; meli hiyo inaaminika ilibeba abiria 800.
Watu 620 walinusurika baada ya kuokolewa ambapo zaidi ya watu 100 hawakujulikana waliko. Meli hiyo ilikuwa ikirejesha watu Pemba kutoka Dar es Salaam na Zanzibar baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.
Mpaka jana jioni zaidi ya miili 20 ya abiria waliofariki dunia iliopolewa ambapo ilielezwa kuwa meli hiyo ilizama baada ya kupigwa na mawimbi makali yaliyosababishwa na kuchafuka kwa bahari kulikotokana na kuvuma kwa upepo mkali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Aziz Juma alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa juhudi za kuokoa abiria zaidi zilikuwa zikifanyika katika Bandari ya Malindi ambapo abiria walionusurika walikuwa wakiletwa hapo baada ya kuokolewa.
Imeshuhudiwa meli inayomilikiwa na Shirika la Bandari ikiwa na maiti 12 pamoja na watu waliojeruhiwa wakiwemo raia wa kigeni 12 ambao wanahisiwa kuwa ni watalii.
Abiria waliojeruhiwa walipelekwa moja kwa moja katika hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi.
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Hamad Masoud alipendekeza boti ndogo zisitishe safari za kwenda Zanzibar au kutoka Zanzibar kwa siku mbili kwa kuwa hali ya bahari ilikuwa mbaya.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi alisema juhudi zinafanywa kuokoa watu waliomo katika meli hiyo kwa kupeleka vyombo zaidi.
Issa alisema juhudi hizo zinafanywa kwa pamoja kwa kuwashirikisha waokoaji kutoka Kikosi cha Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), Shirika la Bandari na Polisi huku boti zinazomilikiwa na kampuni
ya Azam zikisaidia.
Mfanyakazi mmoja mtumishi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko aliyejitambulisha kwa jina la Mkweche, alisema alishuhudia ajali hiyo wakati akiwa katika boti Sea Bus 2 iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam ambapo waliipita boti hiyo huku ikiwa katika mazingira ya kuzama.
"Sisi tuliishuhudia ajali ile na tuliipita ikiwa ipo katika
mazingira ya kuzama baada ya kupigwa mawimbi kutokana kuchafuka kwa bahari.
Mkweche alisema hali ya bahari ilichafuka kwa kiwango kikubwa tangu wakiondoka katika Bandari ya Dar es Salaam hadi walipofika Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi alifika katika Bandari ya Malindi kujionea juhudi za kuokowa watu waliosalimika na ajali hiyo.
Katika hatua nyingine, kuchafuka kwa hali ya bahari kulisababisha baadhi ya abiria katika meli zingine zilizofanya safari katika Habari ya Hindi kupiga simu kwa ndugu zao wakiomba dua ili wafike salama.
Miongoni mwa abiria walioomba dua kutokana na upepo na mawimbi makali ya bahari ni Gloria Shirima, mama aliyekuwa na watoto wawili waliokuwa wakisafiri na meli ya Zanzibar One wakitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar.
Kwa mujibu wa ndugu wa mama huyo, meli hiyo ilikumbwa na upepo mkali uliosababisha ikaribie kupinduka na maji kuingia ndani hali iliyowashtua na kusababisha abiria wengi kuanza kupiga simu kwa ndugu zao kwa ajili ya kuwaombea safari salama.
"Tumepigiwa simu na ndugu yetu, sisi tupo Moshi, yeye yupo na watoto wake wawili, aliondoka Dar es Salaam saa tisa kwenda Zanzibar, anasema bahari imechafuka na meli yao inayumba sana kutokana na upepo mkali, inawezekana hali hii imechangia hata meli hiyo nyingine (MV Skagit) kuzama," alisema dada huyo ambaye hakupenda kutaja jina gazetini.
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na Shirima na ambaye alieleza kuwa mawimbi yalikuwa makubwa na yalileta hofu kwa kila abiria jambo lililowasukuma wapige simu kwa ndugu ili wawaombee na wajue kinachoendelea.
"Nashukuru tumefika salama muda huu huu (saa 11.40), Mungu mkubwa maana hali ilikuwa si nzuri hata kidogo, kweli bahari imechafuka sana leo (jana)," alisema Shirima jana akizungumza na gazeti hili kwa simu.
Wakati shughuli za uokozi zikiendelea kwa shida jana jioni kutokana na kuchafuka kwa hali ya bahari, miili ya abiria 20 waliokufa ilipelekwa katika viwanja wa Maisara na tayari wananchi walianza kupita kutambua ndugu zao.
Shughuli zaidi za uokozi ziliendelea ambapo kwa mujibu wa Sumatra, Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) kilipopata taarifa kuwa meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama.
Baada ya kupata taarifa hizo, kituo cha MRCC kilitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya usafiri wa majini vilivyokuwa karibu na eneo la tukio.
Kwa mujibu wa Sumatra, wadau waliopelekewa tarifa ni pamoja na Polisi Kikosi cha Maji, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha wanamaji, Kituo cha Taarifa Zanzibar na Shirika la Bandari Zanzibar.
Vyombo vilivyokuwa vikisaidia uokoaji kwa mujibu wa Sumatra ni pamoja na meli za Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug, Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I na Boti ya Polisi.

No comments:
Post a Comment