Baada ya kuzagaa taarifa za kupotea kwa mama wa Mfalme wa miondoko ya Pop duniani, Hayati Michael 'Wacko Jacko' Jackson, imefahamika kwamba mama huyo, Katherine yuko kwa binti yake Rebbie na kwamba ameshauriwa na daktari wake kupumzika.
Mwanasheria wa Katherine ametoa taarifa, ikisomeka sehemu, "Wanafamilia wanaohusika, hasa watoto wa Michael wameomba wale wote wanaojua eneo wawajulishe aliko. Taarifa pekee zilizotolewa zimekuwa zikikanganya na kuchanganya hasa zile zinazofungamana na hali ya afya ya Katherine Jackson. Mara ya mwisho kwa watoto wa Jackson walipomwona bibi yao ilikuwa Julai 15, 2012, alikuwa mwenye afya ya kimwili na kiakili."
Aliendelea, "Prince, Paris na Blanket ndio mwanga wa maisha ya Katherine, kama alivyo yeye kwa watoto wake. Mbali na kuwa salama kwa Katherine na katika juhudi za kuhakikisha anakuwa salama kuungana na wajukuu zake mapema iwezekanavyo, taarifa ilipelekwa kwa Idara ya Polisi wa eneo analoishi ambako ndiko utakashughulikiwa uchunguzi wa tukio zima."
Idara ya Polisi ilitoa taarifa iliyosema, "Katherine Jackson ameripotiwa na wanafamilia. Jumamosi usiku, mwanafamilia mwingine aliripoti kwamba hawezi kuwasiliana naye na kwamba anawajibika kwa usalama wake. Wasaidizi wanaendelea kufanya juhudi kumpata na kumwomba awasiliane na Kituo cha Polisi cha Malibu/Lost Hills vilivyoko chini ya Idara ya Mkuu wa Polisi wa Los Angeles."
Katherine aliripotiwa kupotea na mpwa wake usiku wa Jumamosi iliyopita.
Kwa mujibu wa vyanzo, mpwa wa Katherine alitoa taarifa za kupotelewa na mtu kwa Idara ya Polisi baada ya wajukuu zake kushindwa kuwasiliana naye kwa wiki nzima.
Jermaine Jackson alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter wiki hii kwamba Katherine yuko Arizona akiwa mapumzikoni kwa amri ya daktari. Lakini mapema asubuhi, Paris Jackson akatuma ujumbe katika mtandao huo akisema, "ndio, bibi yangu amepotea. Sijaongea naye kwa wiki nataka arudi nyumbani sasa."
Alifuatilia hilo kwa kuomba watu kutoa taarifa kwa mamlaka husika kama wakimwona, kisha akaongeza, "daktari yule yule aliyempima kwa niaba ya dokta Murray akisema baba yangu ameathirika na dawa za kulevya (uongo) ndiye anamhudumia bibi yangu."
Mwanasheria wa Katherine Jackson alieleza hajawahi kupitisha siku bila kuongea na wajukuu zake.

No comments:
Post a Comment