Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imebandika majina yenye orodha ya wasafiri 340 waliokuwa katika meli aina ya Mv Skagit huku wanandugu wakitakiwa kufika kwa ajili ya kuyatambua.
Aidha, polisi jijini Dar es Salaam inamshikilia meneja wa meli hiyo aliyetambuliwa kwa jina la Omar Hassan Mkamnhongt (50) mkazi wa Mgomeni ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Seagul Transport Tawi la Dare s Salaam inayomiliki meli hiyo.
Kadhalika jeshi la polisi, kanda maalum inafanya uchunguzi wa tatizo hilo, wakishirikiana na wadau mbalimbali kusaidia utambuzi wa waliokufa, majeruhi, wabara na wazanzibar pamoja na watalii kutoka nje ya nchi.
Akizungumza jana na baadhi ya wanandugu waliofika ofisini kwake, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik alisema licha ya kubandika orodha hiyo lakini ofisi yake haina uhakika na idadi hiyo kwani huenda walikuwepo zaidi ya hao.
Alisema orodha ya majina hayo itabandikwa katika ofisi zake na kwamba kila mwanandugu anayehitaji kufahamu zaidi anatakiwa kufika na kutambua majina hayo.
Aidha alisema ofisi yake pia inajaribu kuzungumza na wamiliki wa meli au boti ili kwamba waweze kuwasaidia wanandugu wanaotaka kwenda huko ili kwenda kutambua ndugu zao ambao walifikwa na mauti wakati wa ajali hiyo.
"Wapo wanandugu hapa ambao wana uwezo na wanataka kwenda Zanzibar ili kuwatambua ndugu zao, lakini wameshindwa kwenda kutokana na meli nyingine kusitisha usafiri hivyo hao tunakwenda nao bandarini sasa hivi (jana) ili kuwasaidia waweze kufanikisha safari yao," alisema Saidi na kuongeza.
"Kwa wale ambao hawawezi kwenda leo(jana) tutahakikisha tunafanya utaratibu ili kesho (leo) waweze kwenda kwa ajili ya kutambua maiti.
Kuhusu usalama wa meli hiyo, Sadiki alisema kwa mujibu wa taarifa za ukaguzi wa meli hiyo inaonesha kwamba ilikaguliwa 24 Agosti mwaka jana na kwamba ilikuwa inamalizika muda wake Agosti 23, mwaka huu.
"Si kweli kwamba meli ilikuwa haijafanyiwa uchunguzi… polisi wanafuatilia zaidi… na kuanzia leo (jana) tunatengeneza fomu maalum yenye jina la aliyepotea na anayetaka kwenda Zanzibar kutambua maiti ambapo ataandikisha jina lake kwa Edward Mbanga aliyeko katika kofisi za mkuu wa mkoa," alisema.
Kwa upande wake, Kamishana wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, kamanda Suleiman Kova alisema juzi walituma kundi kubwa kwa ajili yakusaidia shughuli ya kuokoa.
Hata hivyo aliwataka wanandugu kuorodhesha majina ya wanandugu wanaohofia kuwa walikuwepo katika meli hiyo, nguo walizokuwa wamevalia ili kwamba kikosi chake kikishirikiana na Mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra) walioko eneo la ajali kusaidia kutambua.

No comments:
Post a Comment