Huku maisha ya June Barnett yakiteketea hospitalini, familia yake inanayompenda mno inaamini kwamba alikuwa akihudumiwa kwa hadhi aliyokuwa akistahili.
Lakini saa moja tu kabla ya kufariki, mtoto wake wa kiume aliwasili kando ya kitanda chake na kukuta mafundi wakiendelea na kazi ya kutoboa matundu ukutani kwa ajili ya kuweka kasha la kushikilia televisheni.
Kitanda cha mjane huyo mwenye miaka 76 kilisukumwa huku na kule na mipira yake ya oksijeni na dripu viliviringwa nyuma ya kiti.
Makasha ya vifaa na ngazi ziliburuzwa kwa sauti sakafuni katika chumba binafsi alikolazwa bibi huyo kwenye Hospitali ya Worcestershire Royal.
Colin Barnett alisema kuwa alimkuta mmoja wa mafundi akiwa ameketi upande wa kichwani juu ya kitanda cha mgonjwa wake huku akiendelea na kazi ya kutoboa matundu.
"Nilisikitishwa mno," alisema. "Niliingia na sikuwa na imani kabisa.
"Ilionekana kama jengo linalojengwa. Usingeweza kutumia vifaa vya tiba maana walikuwa wakikatiza mara kwa mara mbele ya mgonjwa.
"Niliingia na na kuona ngazi na vifaa kadhaa vinavyotumika kwa uvunjaji vikiwa vimetapakaa chini. Walisukuma kitanda chake huku na kule na kuweka mipira yake ya oksijeni nyuma ya kiti.
"Wakati huo alikuwa katika hali mabaya. Nilianza kuhoji kilichokuwa kikiendelea na kuwatoa nje. Kwanini mafundi walikuwa mle ndani, sifahamu.
"Muda mfupi baada ya hapo wafanyakazi walimhamishia chumba kingine na kunieleza kwamba anakaribia kufa. Alikufa saa moja baada ya kuhamishwa.
"Hospitali ilisema mafundi walikuwa mle nusu saa kabla sijawasili. Walikuwa watatu mle ndani, wawili kati yao walikuwa wakipiga soga huku wakimtazama mwenzao akitoboa matundu ukutani.
"Kulitapaa misumari kila mahali kwenye sakafu na vumbi la matofali kutokana na kazi ya kutoboa matundu."
Bibi Barnett, ambaye ana watoto watatu, wajukuu sita na vitukuu watatu, alikuwa akiendesha biashara yake ya upambaji nywele kabla ya kustaafu katika miaka ya 1990.
Mumewe Brian, pia alikuwa mtaalamu wa kupamba nywele, alifariki zaidi ya miaka 10 iliyopita na aliishi kwenye makazi maalumu mjini Worcester.
Alilazwa hospitalini hapo kwa matatizo ya tumbo na kifua na kufariki siku sita baadaye kutoka na nimonia.
Mtoto wake wa kiume mwenye miaka 54 ambaye ni mfanyakazi wa Halmashauri aliongeza: "Sielewi jinsi wataalamu wanavyoweza kuruhusu watu binafsi kufanyi hivyo. Huwezi kuamini, wameshindwa mawasiliano na uangalizi. Inakera sana.
No comments:
Post a Comment