Wabunge wameendelea kutaja mtandao wa uhalifu wa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo Mbunge wa Micheweni Haji Khatib Kai (CUF) alimtaja Kamishna wa Uhamiaji, Peniel Mgonja kwa kutumia madaraka yake kulazimisha askari kutoa hati ya kusafiria kwa raia wa kigeni.
Pia Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli (Chadema) aliishutumu Polisi kwa kutowachukulia hatua askari wanaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo, huku akimtolea mfano aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe (OCD) akimtaja kwa jina moja la Kwayu, kwa kuhusika na matukio mengi ya uhalifu wilayani humo lakini akaishia kuhamishwa.
Juzi, katika mfululizo wa kutaja uhalifu wa watendaji chini ya wizara hiyo, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) alimtaja Fadhili Kweka kuwa askari anayeongoza mtandao wa majambazi.
Akichangia bajeti ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbunge Kai alisema Kamishna Mgonja alimlazimisha askari wa Uhamiaji atoe hati ya kusafiria kwa raia wawili wa Rwanda na kumtishia askari huyo kwamba asipofanya hivyo, atahamishiwa Kijiji cha Ntambaswala, Mtwara.
"Peniel Mgonja namtaja hapa ndani, amekuwa akidhalilisha askari wa chini wafanye mambo kinyume na maadili ya kazi zao, naomba Waziri atakapojibu hoja zetu anieleze atamchukulia hatua gani huyu," alisema Kai.
Mbunge huyo pia aliliambia Bunge namna askari Polisi aliyemtaja kwa namba E 3543 Koplo Ally Faki alivyotelekeza na kumdhalilisha mtoto wa kaka yake hotelini baada ya kulala naye, hali iliyosababisha binti huyo wakati anashuka ngazi kuanguka kwa kiwewe na kuvunjika mguu.
"Baada ya tukio hili, tuliripoti Polisi na binti yule alipopelekwa hospitalini na kupimwa daktari alithibitisha kufanyiwa ubaya, lakini mpaka sasa ninavyoongea hapa, askari huyu hajachukuliwa hatua yoyote na anaendelea na kazi kama kawaida," alisema.
Machemli, alisema inafahamika nchini kote kwamba kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, hali ambayo alisema sasa imekuwa tofauti kwa wakazi wa Ukerewe, kwani mwaka 2009 watu 15 walipoteza maisha katika tukio la ujambazi ambapo polisi walihusishwa na ushahidi anao.
Alisema katika wilaya hiyo yalitokea matukio mengine ya ujambazi na udhalilishaji wananchi kwa kuvuliwa nguo huku Kwayu akishuhudia, lakini baada ya mwezi, kiongozi huyo na maaskari wanaodaiwa kuhusika na matukio hayo walihamishiwa vituo vingine vya kazi.
Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) alidai kuweka mtego wa rushwa dhidi ya askari Polisi Pemba ambao walikamata watu wawili na kwenda nao porini ambako waliwatisha kuwa wataishia jela hadi watakapotoa rushwa.
"Watu wale mmoja ni jamaa yangu, walihaha kutafuta fedha ikabidi wanifuate, nikatoa fedha za mtego, lakini kwa bahati mbaya walishituka na kukimbia, tuliwaripoti hadi leo hawajachukuliwa hatua yoyote na wanaendelea na kazi kama kawaida," alisema.
Mbunge wa Viti Maalumu, Naomi Kaihula alilitaka Jeshi la Polisi kutambua wajibu na dhamana yake kwa Watanzania bila kuegemea upande wa chama chochote katika utendaji wake.
"Hali ya sasa inaonesha kuwa matumizi ya nguvu ya Polisi ni makubwa, polisi wanaogopwa; wanapokamata hata kibaka hutumia silaha kali za moto, lakini pia kuna tatizo la polisi kujihusisha na siasa, vitu hivi viwili vinapaswa vitengane kwani ni tishio kwa usalama wa nchi," alisema Kaihula
Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msabaha (Chadema), alihoji juu ya maadili ya viongozi wa Polisi na Usalama wa Taifa akisema kwa sasa maadili yanaporomoka kwa kuwa nyaraka za siri zimekuwa zikivujishwa hadi kwa raia.
Alisema pamoja na kuvuja kwa siri za ndani za vyombo hivyo viwili muhimu, pia maadili ya askari wake yamekuwa yakiporomoka, kwani kuna wanaofikia kwenda baa wakiwa na sare za kijeshi na silaha.
"Huku ni kuhatarisha maisha ya watu na ndiyo maana tunasisitiza maaskari wote wajengewe nyumba ndani ya kambi, wanapokuwa uraiani hujiingiza kwenye uhalifu, juzi kuna askari alidaiwa kuiba bati, jamani bati askari unaiba si kulidhalilisha Jeshi la Polisi huku?" Alihoji.

No comments:
Post a Comment