KIFO CHA MWANAE CHAMCHANGANYA RAMBO...

KUSHOTO: Sage akiwa katika picha ya pamoja na mpenzi wake na baba yake, Stallone. JUU: Sage akiwa na baba yake, Stallone katika filamu ya Rocky V. CHINI: Eneo la tukio nje ya nyumba aliyokuwa akiishi Sage baada ya kifo chake. KULIA: Sage wakati wa uhai wake.
 Sylvester Stallone au maarufu kama Rambo 'ameumizwa' na 'kujawa na huzuni' baada ya kijana wake Sage kukutwa amekufa mapema jana.
Ripoti zimesema vidonge alivyopewa hospitali vimekutwa eneo la tukio nyumbani kwa kijana huyo mwenye miaka 36 mjini Los Angeles ambamo mwili wake uligunduliwa.
Mtengenezaji filamu imefahamika kwamba alijizidishia dozi ya vidonge na maofisa wa ofisi ya mkemia mkuu wanachunguza kama ilikuwa ajali au jaribio la kujiua, kwa mujibu wa ripoti.
Chanzo kimoja cha habari kimesema kwamba madaktari waliwasili eneo la tukio majira ya saa 9:05 alasiri na kutumia takribani dakika 25 kujaribu kuokoa maisha ya Sage kabla ya kifo chake kutangazwa rasmi eneo la tukio.
Mwili wake ulipelekwa moja kwa moja ofisi ya mkemia na watu wa ndani ya ofisi hiyo wamedai halikuwa tukio la jaribio la kujiua.
"Ninahisi alifariki kitambo kirefu kabla hajagundulika," chanzo cha habari kimeeleza.
"Kwa kawaida madaktari wanakaa katika eneo la tukio kwa dakika 45 lakini waliondoka pale ndani ya dakika 30.
"Kulikuwa na chupa kadhaa za dawa zilizokutwa eneo la tukio lakini haioneshi kama ni kujiua na hakuna waraka wowote uliokutwa."
Simu ya dharura ilipigwa muda mfupi kabla ya Saa 9 alasiri na mpigaji alisema Sage hakuwa akipumua na iliashiria kajizidishia dozi ya dawa, imeripotiwa.
Uchunguzi rasmi wa mwili umepangwa kufanyika katika masaa 48 yajayo.
Muda mfupi baada ya taarifa za kifo cha Sage, msemaji alitoa taarifa kwa niaba ya baba yake shujaa wa filamu za mikikimikiki, mwenye miaka 66, ambaye alikuwa kwenye mkutano wa Comic Con Film mjini San Diego juzi.
"Sylvester Stallone ameumizwa na kuhuzunishwa kufuatia kifo cha ghafla cha kijana wake," msemaji wa mwigizaji huyo Michelle Bega alisema katika taarifa yake.
"Huruma yake na mawazo yako pamoja na mama wa Sage, Sasha."
"Alikuwa na kipaji sana na kijana wa ajabu. Pengo lake halitazibika milele."
Polisi wamesema walimkuta Stallone mtoto nyumbani wakati walipokuwa 'wakikagua ustawi wa jamii', licha ya taarifa za Mwanasheria wa Sage, George Braunstein kwamba aligunduliwa na mfanyakazi wa ndani.
Marafiki wameguswa sababu hawakumsikia Sage siku nzima iliyopita.
Braunstein alisema kifo kimekuja kama mshituko, akieleza mchana huu: "Alikuwa na roho nzuri, na kufanya kazi katika kila aina ya miradi.
"Alipanga kuoa. Nimeumizwa sana. Alikuwa wa ajabu sana, kijana mwenye upendo. Hili ni janga."
Sage Moonblood Stallone alikuwa mtoto mkubwa wa Sylvester Stallone na alishiriki kama nyota-mwenza kwenye filamu mbili za baba yake. Alikuwa mtoto wa kwanza kati ya watoto wawili wa kiume wa Stallone aliozaa na mke wa kwanza, Sasha Czack.
Alianza kazi yake ya uigizaji mwaka 1990 kwenye filamu ya Rocky V, akicheza kama mtoto wa Stallone, na pia akacheza tena na baba yake mwaka 1996 katika Daylight.
Pia mwaka 1996, Sage Stallone na mkongwe wa uhariri filamu, Bob Murawski walianzisha kampuni Grindhouse Releasing, iliyojihusisha na
kutunza na kupromoti B-movies na filamu za uchimbaji za kati ya miaka ya 1970 na 1980.
Pia aliongoza filamu fupi ya Vic mwaka 2006, ambayo ilioneshwa kwenye Tamasha la Filamu la Palm Springs.
Braunstein alisema Sage alikuwa na maombi mengi ya mara kwa mara ya kazi za kucheza filamu.
Aliongeza kwamba Sage Stallone alikuwa akimzimia mno baba yake lakini alikuwa akifanya juhudi kubwa kujipambanua kivyake kwenye tasnia ya filamu.
"Alikuwa akisikia fahari sana kwa baba yake na kuwa mtoto wa baba yake," alisema.
Stallone alitengana na mama wa Sage, Czack mwaka 1985 baada ya kuishi pamoja kwa miaka 11.
Pia wana kijana mwingine Seargeoh mwenye miaka 32, ambaye ana matatizo ya akili.
Akamuoa mwanamitindo na mwigizaji wa kike Brigitte Nielsen Desemba mwaka uliofuata huko Beverly Hills lakini wakatengana miaka miwili tu baadaye katika talaka ya wazi.
Alioa mke wa tatu, Jennifer Flavian mwaka 1997 baada ya miaka minane mahusiano ya kurudiana na kutengana na wana mabinti watatu: Sophia Rose mwenye miaka 15, Sistine Rose mwenye miaka 14 na Scarlet Rosw mwenye miaka 10.
Sage, ambaye amelelewa na mama yake baada ya kutengana kwa wazazi wake, alikuwa mbali na baba yake wakati wote wa kukua kwake, jambo lililoisumbua familia yake wakati wakiigiza Rocky V pamoja.
"Pale nilipopiga kelele kulalamika, "Hukuwa na muda kukaa nami! Hukujipa muda kukaa na mama yangu!" - ile ilikuwa kweli," aliliambia jarida la People mwaka 1996.
"Nilitazama sura ya baba yangu na hakika nilisema kwa dhati."
Lakini ilithibitisha wakati wa mabadiliko kati ya baba na kijana wake, ambao walikwenda kuunda ukaribu na kuigiza tena pamoja mwaka 1996 filamu ya Daylight.

No comments: