JUSTIN BIEBER AKAMATWA KWA KUENDESHA GARI KIZEMBE...

Mwimbaji Justin Bieber amenaswa akiendesha kwa kasi kubwa gari lake tena bila tahadhari yoyote, ndipo shuhuda mmoja ambaye anaaminika ni mfanyakazi wa halmashauri ya jiji la Los Angeles alipopiga simu polisi, imeelezwa.
Mfanyakazi huyo Dennis Zine ambaye aliwahi kuwa Ofisa Usafiri wa Kitengo cha Polisi cha Los Angeles kwa miaka 18, alikuwa katika njia namba 101 ndipo alipomuona Justin kwenye njia yake inayoelekea Fisker Karma akishusha kwa kasi ambayo Zine anasema ni zaidi ya maili 100 kwa saa.
Zine ameeleza kuwa Bieber alikuwa akijaribu kuwatisha waandishi wa habari ambao walikuwa wakimfuatilia.
Zime amesema, "Bieber alikuwa akiendesha kasi kama mwenye wazimu. Alikuwa akichora herufi 's' barabarani kwa kuchomeka gari kushoto na kulia."
Zine aliongeza, "Kama ningekuwa kwenye doria enzi zangu, ningemkamata kwa uendeshaji gari kizembe. Nilikuwa nikiendesha kwa spidi 60 na akanipita kama vile alikuwa kwenye roketi. Alikuwa na wazimu."
Alisema kuwa waandishi wa habari nao hawakutimiza wajibu wao kwa kuendesha ovyo na kusababisha hatari kubwa.
Baada ya kusimamishwa, waandishi karibu wanne wakavamia gari la Bieber.

No comments: