JAJI 'MTATA' SASA ARUHUSU MBAKAJI KUBAKI UINGEREZA...

KUSHOTO: Binti wa miaka 12 ambaye alibakwa. KULIA: Jaji Jonathan Perkins.
Mkimbizi kutoka Sudan anayetaka hifadhi ya kisiasa ambaye alimbaka msichana wa miaka 12 ameruhusiwa kubakia Uingereza baada ya Jaji kutoa hukumu kwamba kumfukuza itakuwa ni kuvunja haki za binadamu.
Sani Adil Ali alifungwa kwa kosa la kumbaka msichana miezi kadhaa baada ya kupatiwa hadhi ya ukimbizi.
Wakati alipohukumiwa, jaji mwingine alimuelezea kama 'hatari dhahiri kwa wasichana wadogo' na kumuweka kwenye orodha ya wabakaji kwa maisha yake yote.
Lakini baada ya kutumikia kifungo chake cha miaka mitatu, mahakama inayohusika na masuala ya uhamiaji ilihukumu kwamba Ali abakie Uingereza kwa maelezo kwamba atakuwa hatarini endapo atarejeshwa Sudan.
Jaji wa ngazi ya Juu wa Uhamiaji Jonathan Perkins alimruhusu kijana huyo mwenye miaka 28 kubaki Uingereza, ingawa maofisa wanaoshughulikia kesi za ubakaji wamemuona atasababisha madhara kwa watoto.
Katika hukumu yake, Jaji Perkins alisema: "Tumegundua kwamba mlalamikaji bado yuko kwenye ulinzi katika Mkusanyiko wa Wakimbizi na ana hadhi hiyo.
"Kwa vyovyote, kumuondoa kutakinzana na makubaliano ya Uingereza kwenye Mkataba wa Ulaya kuhusu Haki za Bianadamu."
Hii si mara ya kwanza kwamba Jaji Perkins amefanya maamuzi yenye utata. Mwezi uliopita, iliripotiwa jinsi jaji huyo alivyoruhusu Muislamu wa Afghanistan, ambaye alidaiwa kuua watu akilitumikia kundi la Taliban, kubakia Uingereza.
Iliripotiwa pia kwamba Jaji Perkins pia aliruhusu watuhumiwa wa kimataifa kubaki Uingereza sababu ya 'haki kwa maisha ya familia' chini ya Sheria ya Haki za Binadamu.
Uamuzi wake wa hivi karibuni kabisa ni pingamizi lingine kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Theresa May, ambaye alipanga kutengua kipengele ambacho watuhumiwa wamekuwa wakitumia haki za binadamu kukwepa kurejeshwa makwao ambapo kimekuwa kikitumiwa sana na mahakama.
Mbunge wa Dover & Deal wa chama cha Conservative, Charlie Elphicke, ambaye aliwasilisha muswada kubadili Sheria ya Haki za Binadamu na Muswada wa Haki za Uingereza, alisema: "Uingereza itaendelea kuwapo kutoa fursa kwa wakimbizi wote wanaohitaji hifadhi. Lakini watu wanaofanya uhalifu hapa wanatakiwa kutimuliwa haraka sana.
"Watu wanaofikiri kwa usahihi katika Uingereza watakubaliana kuwa mtu huyu anaruhusiwa kubaki hapa. Inajumuisha kilichokosewa kwenye sheria za haki za binadamu za Ulaya.
"Hatutakiwi kuwa na huruma kwa wakimbizi wanaofanya uhalifu. Kesi kama hizi ndio sababu ya mimi kuwasilisha Muswada wa Uingereza wa Haki hivyo kudhibiti mipaka yetu na kuhakikisha wahalifu kutoka nje na magaidi wanarejeshwa makwao haraka sana."
Ali alimshambulia msichana mwenye miaka 12 wakati akiishi na familia ya binti huyo katika ziara yao ya siku tano huko Sheffield. Familia ya muathirika walimkaribisha wakati alipokwenda kumtembelea rafiki yake, Kamel Ahmed, ambaye wakati huo alikuwa na miaka 22, pia kutoka Darfur.
Ali ambaye anatokea mkoa wa Darfur, aliwasili Uingereza Oktoba 2003 na akapatiwa hadhi ya ukimbizi Februari 2005.
Lakini miezi miwili baadaye alikamatwa katika makazi yake mjini Middlesbrough kwa tuhuma za kumbaka msichana huyo mwenye asili ya Hungary.
Ali na Ahmed walikuwa wakifahamiana na familia ya msichana huyo kutoka kwenye kambi ya wakimbizi nchini Italia na Ufaransa.
Ali, ambaye alipatikana na hatia kwenye moja ya mashitaka yake ya kubaka mtoto, alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela katika Gereza Kuu la Sheffield.
Ahmed yeye alikutwa na hatia kwenye mashitaka matatu ya kubaka mtoto na alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.
Wakati Ali alipoachiwa kutoka Gereza la Doncaster mwaka 2008, Wizara ya Mambo ya Ndani iliamuru kwamba arejeshwe Sudan na alifungiwa kwenye kituo maalumu cha Uhamiaji kwa ajili watu wanaongojea kurejeshwa makwao.
Ali alikata rufani katika Mahakama ya Uhamiaji ambapo Jaji alitupa pingamizi lake, ndipo alipokata rufani kwa Mahakama ya Juu ya Uhamiaji na Ukimbizi.
Katika mahakama hiyo, Jaji Perkins aliamua kwamba kumuondoa Ali, ambaye anatokea kabila la Zaghawa, kungevunja haki yake Chini ya Kifungu 3 cha Makubaliano ya Ulaya kuhusu Haki za Bianadamu, ambacho kinakataza mateso au adhabu za kinyama.
Jaji Perkins alirejea hukumu ya 2009 ambayo ilisema kwamba makabila yasiyokuwa ya Kiarabu kama Zaghawa yamo 'hatarini huko Darfur na kwamba hayawezi kuishi kokote kule nchini Sudan".
Alipoulizwa Wakala wa Mipaka wa Uingereza alisema: "Watuamini mtu huyu anahitaji ama anastahili kuwa mkimbizi katika nchi hii."

No comments: