FAMILIA YAMUUA MJAMZITO KWA IMANI ANAONGOZWA NA SHETANI...

Wanafamilia wanne wamekutwa na hatia ya mauaji ya mwanamke mjamzito mwenye miaka 21 ambaye walifikiri kuwa anaongozwa na roho za kishetani.
Kufuatia kesi iliyonguruma kwa wiki 12 kwenye Mahakama ya Birmingham, mume wa Naila Mumtaz, Mohammed Tauseef Mumtaz, mwenye miaka 25, wazazi wake, Zia Ul-Haq na Salma Aslam, wote wakiwa na miaka 51, na shemeji yake, Hammad Hussan mwenye miaka 24, walikutwa na hatia ya kumuua.
Wazee wa baraza la mahakama walielezwa kwamba Mumtaz, ambaye anashitakiwa kwa kumkaba koo mkewe aliyekuwa mjamzito wa miezi sita, aliwaeleza polisi kuwa mke huyo alikuwa akijaribu kujinyonga na inawezekana alikuwa 'akiongozwa' na roho za kishetani.
Mahakama ilielezwa kwamba alidai kifo cha mkewe kilikuwa kama cha 'kujitoa muhanga' na kwamba alishikiliwa kama hivyo kwenye mahakama ya jiji hilo baada ya kifo chake.
Washitakiwa wote wanne wamekana mashitaka ya mauaji ya Naila nyumbani kwake huko Mtaa wa Craythorne, Handsworth Wood, mjini Birmingham, mapema Julai 8, 2009.
Wakili Wendy Bounds kutoka Kampuni ya Uendeshaji Mashitaka ya West Midlands alisema: "Naila Mumtaz, msichana mrembo mkarimu alikuwa akiishi nchini Pakistan pamoja na wazazi wake, alikubali kuingia kwenye ndoa na mtuhumiwa, Mohammed Tauseef Mumtaz.
"Alijua kwamba alikuwa na kasoro za kimaumbile, lakini hakutatizwa na muonekano wake huo, akamchukulia kwa upendo kwamba viumbe hai wote wanathamani sawa.
Hatahivyo, leo imegundulika kwamba mumewe na familia yake hawakumpa thamani hiyo Naila.
"Naila alikuwa mjamzito wa miezi sita na alikuwa akiishi na watuhumiwa mjini Birmingham ndipo Julai 8, 2009 familia ikapiga simu ya dharura kuita gari la wagonjwa nyumbani hapo.
Juhudi zote kuokoa maisha yake zilizofanywa na madaktari nyumbani hapo na pia hospitalini zilishindikana, ndipo yeye na mtoto aliyekuwa tumboni wakafariki dunia.
"Aligundulika kuwa na majeraha na jaji alilazimika kuamua kama aliuawa, kunyongwa na kuzibwa pumzi na mumewe, wazazi wake na shemeji yake au pengine kama walivyoshikilia msimamo kwamba anaongozwa na roho za kishetani ndizo zimechukua uhai wake."
Wakati wa kusoma maelezo ya awali, Mwendesha Mashitaka Christopher Hotten QC alinukuu maelezo ya Mumtaz aliyoandika polisi baada ya kifo cha Naila, akisema: "Alisema Naila alianza kujikwaruza uso wake na alikuwa akilia kwa hasira.
"Alijaribu kutafuna mkono wa mama yake. Familia nzima ilikuwa ikijaribu kumtuliza.
"Ni kama vile alikuwa hatukumbuki sisi kina nani. Alijiziba pumzi mwenyewe kwa kuingiza mkono wake mdomoni na alijaribu kujinyonga mwenyewe.
Katika maelezo yake polisi, Mumtaz aliendeleza msimamo wake kwamba majeraha katika mwili wa mke wake yalitokana na kujidhuru mwenyewe na alidai kwamba mtu mmoja alikuwapo nyumbani hapo akimuombea "kumtoa pepo huyo mchafu ndani yake".

No comments: