DOKTA MURRAY BADO ASAKA NAFASI KUTHIBITISHA HAJAMUUA MICHAEL JACKSON...

Dokta Conrad Murray anaamini ana nafasi ya kuthibitisha kwamba Michael Jackson alijidungwa mwenyewe sindano katika sakata la kujizidishia dozi ya Propofol, na sasa anaomba pingamizi mahakamani kuthibitisha hilo.
Wanasheria wa Murray wanafungua mjadala mpya kwenye pingamizi, wakidai kichupa kidogo cha Propofol kinaweza kubeba ushahidi wa kutokuwa kwake na hatia …ikiwa tu Jaji ataruhusu uchunguzi wa kina kujua uwepo wa dawa aina ya lidocaine.
Lidocaine ni muhimu kwa sababu upande wa mashitaka umelumbana kwamba Murray alimwinua Michael Jackson na kumpatia pakiti ya IV iliyokuwa na dozi ya Propofol kisha kumwacha pekee …lakini kwanza, alichanganya Propofol na lidocaine kuongeza ukali wa dawa hiyo.
Murray anadai uchunguzi utabainisha hakukuwa na lidocaine katika kichupa kidogo, sababu Michael Jackson alijidunga mwenyewe kwa kutumia dozi halisi ya Propofol na kujiua mwenyewe.
Murray ambaye alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na sasa anatumikia kifungo katika Gereza Kuu la Los Angeles, tayari ametuma maombi mawili ya kufanyika uchunguzi huo. Yote yalikataliwa na Jaji ambaye aliongoza mashitaka dhidi yake … na kuamua kwamba Murray anatakiwa kuomba kabla kesi mashitaka hajaanza kusikilizwa.
Timu ya wanasheria wa Murray wanatarajiwa kufungua madai wakati wowote kuanzia sasa. Itachukua miezi kadhaa kabla ya mahakama kutoa uamuzi wake.

No comments: