CHIPSI HOLELA ZAPIGWA MARUFUKU MICHEZO YA OLIMPIKI...

Mamia ya vibanda vya chakula katika viwanja vya Olimpiki vimelazimishwa kuachana na kuuza chipsi wakati wa michezo hizo, kutokana na matakwa ya mdhamini McDonald's.
Wakuu wa Olimpiki wamewafungia wauza chakula wa rejareja wote 800 kwenye Viwanja vya Michezo hiyo ya 40 kote Uingereza kuuza chipsi sababu ya 'masharti ya udhamini.'
Upenyo pekee kwenye mkataba, iliyotangazwa katika waraka kwa wafanyakazi, ni kwamba chipsi zinaweza kuuzwa tu zikiwa na samaki, chakula ambacho ni maarufu zaidi nchini Uingereza.
Lakini inaonekana mabosi wamebashiri ugumu wa uamuzi huo, wakisisitiza kwamba uamuzi huo haukushirikisha wauzaji chakula cha rejareja.
Waraka unasomeka: "Kufuatia masharti ya udhamini na McDonald's, Locog imeamuru timu ya usambazaji vyakula hawaruhusiwi tena kuuza chipsi wenyewe popote ndani ya eneo la kijiji cha Olimpiki.
"Upenyo pekee katika hili ni kama zitauzwa zikiwa na samaki."
"Tafadhali tambua hili kuwa huu si uamuzi wa mfanyakazi anayekuhudumia mlo, ambaye anaweza kuchagua kukupatia kwa furaha wakati wamekatazwa kufanya hivyo.
"Hili ni agizo lililopitishwa na wakurugenzi wa L2012C na Locog na OIC.
"Tafadhali msiwape huzunu wafanyakazi, hii itatuongoza tu pale inapokosekana samaki kwenye chipsi.
"Kila mmoja ana haki ya kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa na usumbufu."
Washirika wa kibiashara Coca-Cola, McDonald's, Cadbury, Nature Valley na Heineken zitakuwa bidhaa pekee zitakazoruhusiwa kuuzwa katika michezo hiyo.

No comments: