CHETI CHA KIFO CHA NATALIE WOOD CHABADILISHWA...

Imegundulika kwamba cheti cha kifo cha Natalie Wood kimebadilishwa kutoka "Ajali" na sasa kusomeka "Isiyojulikana".
Vyanzo vya habari vya kisheria vimeeleza kuwa Mkemia Mkuu wa Los Angeles alikabidhi nyaraka akifanya mabadiliko hayo mwishoni mwezi uliopita.
Wanafamilia ya Wood walisema wapelelezi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Los Angeles ambao walianzisha upya uchunguzi wa kifo hicho, walitembelea mapema jana wakiwajulisha kuhusu mabadiliko hayo. Walituambia, wapelelezi waliwaambia mabadiliko yamefanyika kwenye baadhi ya sehemu sababu baadhi maeneo zilipovilia damu hazihusiani na kifo cha kuzama kwenye maji.
Wanafamilia wameongeza... walitueleza katika wakati fulani kwamba mamlaka haziwezi kuthibitisha bayana kifo cha Natalie kilikuwa ajali au kimetokana na hujuma. Wapelelezi waliwaeleza wanafamilia kifo cha Natalie kilikuwa dhahiri kutokana na kuzama kwenye maji, lakini jinsi hasa alivyoishia kwenye maji haijulikani.
Natalie alifariki Novemba 29, 1981 baada ya sherehe iliyoambatana na pombe kibao ndani ya boti kutokea Catalina akiwa na Robert Wagner na Christopher Walken ndani ya boti hiyo.
Vyanzo vya habari vimeeleza uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

No comments: