CHEKA TARATIBU...

Mwanajeshi mmoja akiwa katika vita ya Kagera kahuzunika sana baada ya kupokea barua kutoka kwa rafiki yake wa kike ikielezea kusitisha mpango wao wa kufunga ndoa. Kama haitoshi katika barua akamtaka mwanajeshi huyo arudishe picha yake.
Siku iliyofuata mwanajeshi akapita kwa rafiki zake na kukusanya picha zote za wanawake wenye sura mbaya, akazifunga pamoja kwenye bahasha na kuzituma kwa mwanamke wake akiandika, "Nasikitika kukujulisha kwamba sikumbuki picha yako ni ipi kati ya hizi, tafadhali chagua yako kisha nirudishie zilizobaki." Duh...

No comments: