BILIONEA OPRAH WINFREY KATIKA VITA NA MAMA WA KAMBO...

KUSHOTO: Barbara akiwa na mumewe, Vernon. KULIA: Oprah Winfrey.
Kipindi cha Mahojiano ya Televisheni ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa Marekani cha Oprah Winfrey kimewapa ushauri maelfu ya watu mpaka sasa.
Lakini bilionea huyo anakabiliwa na matatizo yake binafsi baada ya kujikuta kwenye wakati mgumu wenye machungu dhidi ya mama yake wa kambo.
Barbara Winfrey, ambaye ameolewa na baba wa Oprah, Vernon amemtuhumu bilionea mwendeshaji wa kipindi hicho cha maongezi kushinikiza mama huyo kuachana na mumewe.
Amedai Oprah amekuwa akitumia utajiri wake kudhibiti saluni ambayo Vernon amekuwa akiiendesha kwa miaka 50 sasa.
Na sasa baba huyo mwenye miaka 78 amefungua madai ya talaka kwa madai mzozo wa umiliki wa saluni hiyo ukitishia kusambaratisha familia ya Winfrey.
Duka hilo lililopo mjini Nashville, Tennessee, lilinunuliwa na Oprah wiki iliyopita baada ya kuonesha dalili za kutaka kufilisika.
Alilipa Dola za Marekani 475,000 kwa ajili ya mali wakati ambapo ilikuwa kwenye maandalizi ya kupigwa mnada.
Barbara Winfrey amesema kununua saluni inamaanisha mwendeshaji wa kipindi hicho, ambaye kwa sasa anaendesha mtandao wake wa YV, amerejesha nguvu kwenye udhibiti wa biashara hiyo na kumuengua yeye.
"Najua kinachoendelea. Nimechoshwa, na imetosha kwa sasa," alisema Barbara Winfrey alipohojiwa na televisheni ya WSMV mjini Nashville.
Barbara na mumewe mwenye miaka 78 walifungua saluni mwaka mmoja uliopita badala ya duka lililopo jirani na mahali hapo.
Lakini wapenzi hao wameshindwa kulipa mkopo wa nyumba na jengo hilo lililojengwa kwa matofali mekundu likaelekea kufilisiwa.
Barbara alisema alitaka kukopa fedha zaidi kutoka benki lakini kufuatia ushauri kutoka kwa binti yake maarufu, Vernon akakataa kukopa.
"Watu wanamshauri vibaya, na kuniacha mimi mahali ambapo ninachoweza kufanya ni kujipigania mwenyewe," alisema Barbara Winfrey.
"Hakuna sababu yoyote ya kupelekea kufilisika kama hivi. Kitegauchumi kimepinduka kabisa, kama zilivyo mali nyingi. Imetugharimu Dola za Marekani 481,000 kujenga jengo hili, lakini limethaminiwa kwa Dola za Marekani 350,000 tu."
Barbara alivieleza vyombo vya habari kwamba Oprah alikuwa akimwendesha baba yake.
"Anaamini kila anachoambiwa. Binti yake hajali kuhusu jamii. Binti yake hajali kuhusu saluni. Lakini mimi najali," alisema Barbara Winfrey.
Televisheni ya WSMV ilisema wamethibitisha kwamba Oprah, ambaye ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola za Marekani bilioni 2.7, alilipa Dola za Marekani 475,000 kwa ajili ya ununuzi wa saluni hiyo.
Katika taarifa yake kwa kituo hicho cha televisheni, msemaji wa Oprah alisema: "Oprah amenunua kitegauchumi hicho ambacho kilikuwa katika kufilisiwa.
"Vernon Winfrey amekuwa akihudumia jamii kwa miaka kadhaa na ataendelea kumiliki biashara katika utaratibu wa siku hadi siku."
Barbara ameema kwamba mumewe licha ya kufungua madai ya talaka, anaamini haelezi chochote kuhusu uamuzi anaofanya.
Katika mahojiano kwa njia ya simu na kituo cha televisheni, Vernon alisema: "Mke wangu na mimi, hatukuwa tukiiva pamoja na sitaki kujitumbukiza kwenye kunyonywa na kuhangaika kulipa madeni."
Vernon, ofisa wa zamani wa halmashauri ya mji, ameendesha saluni hiyo iliyoko East Nashville kwa miaka 50 sasa.
alihama kutoka majengo ya zamani mwaka 2011 na kufungua saluni mpya.
Wakati wa ufunguzi wa saluni mpya, Vernon alisema saluni mpya itakuwa urithi wake kwa jamii.
"Nitakapokufa, ninafuraha nitaweza kusema nimeacha mazingira jirani ya kupendeza," alisema Winfrey.
Alisema binti yake amemshauri kuachana na kazi ya kinyozi, lakini amepanga kuendelea.
"Baadhi ya jamaa zangu wanasema, "Winfrey wewe sasa ni mzee kufanya kazi hiyo." Nawajibu, "Mko sahihi, lakini najisikia vizuri," amesema.
Vernon anasema kwamba binti yake amekuwa akimtaka kustaafu kazi hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

Oh, what you are doing this prасtice myself, and it's clear that there are a huge improvement, though, this can hasten recovery from diseases. There's аlѕo а floral peeling, detailеd care foг smooth rаdiant skin and shiny,
the hair becomes leѕs coаrse and grows morе erotіс massagerse.
By trying out new outlets οr sаlon with sρeciаl promotіons.



Also ѵisit my weblog :: tantric massage