Watoto watatu waliokutwa wamekufa kwa kuchomwa visu katika eneo lenye mandhari nzuri juzi wanahofiwa kuuawa na baba yao.
Ceri Fuller mwenye miaka 35, anashukiwa kuwaua mtoto wake wa kiume Sam mwenye miaka 12, na binti zake Becka mwenye miaka 8, na Charlotte mwenye miaka 7, kisha na yeye kujiua kwa kujitupa kwenye bonde lenye kina cha futi 80 jirani na alipofanyia mauaji ya watoto wake.
Siku moja kabla ya janga hilo, mama wa watoto hao, Ruth, aliandika kwenye mtandao wa Facebook kuhusu 'wazimu' wa migogoro kwenye maisha ya kati.
Alisema: "Ile migogoro ya maisha yangu ya kati imeisha na mambo machache tu ya kiwazimu yamefanyika."
Mama huyo mwenye miaka 34 aliongeza: Bado, nina furaha ushauri kuwafikia watu, ndicho ninachopenda." Maoni hayo yalikubaliwa na dada wa Fuller, Abigail kupitia mtandao huo.
Msako mkubwa ulifanyika kumtafuta Fuller, mhitimu wa baiolojia ya molekule na selula, baada ya kutoweka ghafla nyumbani kwake Milkwall, mjini Gloucestershire wiki iliyopita.
Watoto walishindwa kurejea shuleni Ijumaa, na Fuller hakutokea kazini kwake ambako ni msimamizi uzalishaji katika kiwanda cha karatasi Glatfelter kilichopo mji jirani wa Lyndey.
Miili yote minne ilikutwa umbali wa maili 75 kutoka nyumbani upande wa jirani na Shrewsbury juzi baada ya gari la Fuller aina ya Land Rover kukutwa limeegeshwa eneo hilo la tukio.
Polisi wanaamini aliwauwa watoto na kujiua mwenyewe Alhamisi, kabla ya kupatikana taarifa za kupotea kwao.
Juzi mwanafamilia alisema Fuller alikuwa katika 'hali ya kutisha' wiki iliyopita lakini alikuwa mgumu sana kufafanua kwa undani.
Majirani walisema walimuona Ruth, msanii, akiwa mwenye mashaka na wasiwasi siku ambayo mumewe alitoweka nyumbani.
Akiongea kwenye mkutano na vyombo vya habari, Inspekta Mkuu wa Polisi Neil Jamieson alisema: "Miili ilipatikana majira ya saa 4 asubuhi katikati ya machimbo ya zamani kwenye eneo la miti huko Poles Coppice.
"Ingawa utambuzi wa kawaida haukufanyika, inaaminika mwanaume huyo ana miaka 35 Ceri Fuller na watoto, Sam mwenye miaka 12, Rebecca miaka 8 na Charlotte miaka 7.
"Naweza kuthibitisha tumeanza uchunguzi wa mauaji na hapa tulipofikia hatutafuti mwingine yeyote anayehusika na tukio hili.
"Inaonekana wazi kuwa ni tukio la janga la kifamilia.
"Miili minne ilikutwa ndani ya yadi 30-40 kutoka mmoja hadi mwingine. Hadi sasa, hatuwezi kusema kama silaha imetukima au kama silaha yoyote imepatikana eneo la tukio.
"Tuna wasiwasi kufuatilia nyendo za Land Rover Freelander nyekundu, yenye usajili CK51 YUV, ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Fuller.
"Gari hili liliripotiwa kuegeshwa kwenye lango la Poles Coppice kiasi cha yadi 300 kutoka eneo ambalo miili ilikuwako.
"Tunaamini liliwasili eneo hili nyakati fulani tangu Alhamisi.
"Tunaamini gari hili liliondoka huko Gloucestershire nyakati fulani Jumatano jioni au mapema Alhamisi asubuhi.
"Mtaalamu wa magonjwa wa Wizara ya Mambo ya Ndani atafanya uchunguzi kusaidia kugundua sababu na muda mauaji hayo yalipotokea. Hiyo ilitarajiwa kufanyika jana au leo.
Fuller alitoweka na watoto wake katika nyumba yao yenye thamani ya Pauni za Uingereza 162,000, ambayo inaaminika alichangia na mkewe na mama wa watoto watatu, Ruth mwenye miaka 34.
Jirani alisema alimuona Ruth ambaye alioana na mumewe mwaka 2009, mwenye mashaka akirandaranda barabarani nje ya nyumba yake siku ambayo mumewe na watoto walitoweka.
Mmiliki wa zamani wa nyumba hiyo ya Fuller ambaye hakutaka kujitambulisha alisema: "Hakuwa mtu mgomvi kabisaa, mkewe siku zote alipenda kuvalia suruali, na walikaa kivyao."
Ilifahamika kuwa mfanyakazi huyo wa kiwanda cha karatasi alikuwa akiwapeleka watoto wake safari ya Barmouth au Harlech, kaskazini-magharibi mwa Wales, ambako siku za nyuma walikuwa mapumzikoni.
Mama wa Fuller, Geraldine mwenye miaka 64 na baba yake wa kambo, Geoffrey Petheram ambao wanaishi jirani na hapo katika eneo la Blackeney, walihuzunushwa na kushitushwa mno na taarifa za janga hilo.
Wazazi we Ruth, Anne an Ronald Tocknell hawakuwapo nyumbani kwao katika mat wenye nays nyingi hook Lydney, Gloucestershire.
No comments:
Post a Comment