Nesi amemchoma visu hadi kufa binti yake wa miaka minne na kujaribu kujiua mwenyewe kwa kunywa dawa ya kuondoa madoa baada ya kukabiliwa na adhabu ya kufukuzwa kazi kutokana na kuvujisha siri za mgonjwa kwa kampuni ya wanasheria wanaoshughulika na ajali ya "cash and claims'.
Dawn Makin mwenye miaka 33, ambaye kwa sasa anatembea kwa msaada wa kiti chenye magurudumu kufuatia jaribio lake la kutaka kujiua, alivunja kiapo chake kama mhudumu wa afya pale alipovujisha kwa siri taarifa nyeti kwa rafiki yake wa kiume ambaye alikuwa akijaribu kusainisha wagonjwa malipo binafsi ya fidia ya ajali.
Lakini mabosi wa afya walichunguza kashfa hiyo, Makin ambaye anakabiliwa na adhabu ya kupoteza kibarua chake, akamchoma visu Chloe Burke hadi kufa na kisha kukata kifungo cha shati na kunywa kimiminika chenye sumu, inayoaminika kuwa ni dawa ya kuondoa madoa, katika harakati za kutaka kujiua.
Jana, kwenye mahakama ya Preston, alimwaga machozi baada ya kupatikana na hatia ya mauaji kwa kushindwa kutimiza wajibu baada ya ombi lake la 'kutokuwa na hatia ya mauaji' kukubaliwa na upande wa mashitaka.
Alikutwa akiwa taabani kando ya mwili wa Chloe nyumbani kwao Fairfield, Bury, huko Greater Manchester baada ya ndugu mwenye mashaka kumtaarifu jirani.
Makin alikimbizwa hospitali akiwa hajitambui na baadaye akapata fahamu kidogo lakini kwa miezi kadhaa alionekana kuzidi kuwa dhaifu sana kiasi cha kushindwa kuhojiwa na polisi.
Alishitakiwa kwa mauaji miezi kumi baadaye lakini sasa anatumia kiti cha magurudumu na anaishi chini ya uangalizi kwa saa 24 katika kitengo cha kurekebisha tabia kilichopo hospitalini hapo. Uchunguzi umebaini Chloe alikufa kutokana na majeraha kadhaa ya kuchomwa na kisu.
Atahukumiwa mwezi ujao kufuatia maandalizi ya ripoti mbili kutoka kwa mtaalamu wa magonjwa ya akili na ameachiwa kwa dhamana.
Wanasheria wanatarajiwa kutoa matamko kutoka kwa familia ya Chloe na kukabidhi picha za eneo la mauaji na majeraha ya binti huyo mdogo wakati ujao wa usikilizwaji shauri hilo. Baba wa Chloe, Michael Burke hakuwapo mahakamani.
Janga hilo lilitokea wakati Makin alipoonywa kwamba atakabiliwa na adhabu za kinidhamu na kufukuzwa kazi kwa kutumia kompyuta ya kituo cha Moorgate Primary Care kinyume cha sheria ambako alikuwa akifanya kazi mjini Bury.
Mapema alikuwa chini ya uchunguzi wa Ofisi ya Kamishna wa Mawasiliano kwa kuvujisha taarifa za mgonjwa kwa mpenzi wake Martin Campbell ambaye wakati huo alikuwa akifanya kazi kama wakala wa kampuni inayoshughulika na madai ya majeraha binafsi ya Direct Assist.
Campbell mwenye miaka 34, alipata majina na simu 29 za waathirika wa ajali ambao walikuwa wakitibiwa kituoni hapo na kuwasiliana nao mwenyewe katika harakati za kusaini nao na kujiongezea malipo kwa kipindi cha zaidi ya miezi minne tangu Desemba 2009.
Alikamatwa baada ya wagonjwa kuanza kulalamika kwa Shirika la Taifa la Afya (NHS) huko Bury, wakisema kwamba kuna mtu amewapigia kuhusu majeraha yao na kuwahamasisha kufungua madai yao binafsi.
NHS kisha ikachunguza na kugundua mafaili yamekuwa yakishughulikiwa na Makin bila sababu zozote halali.
Mwili wa Chloe ulipatikana Februari mwaka jana baada ya bibi yake, Sheila Makin, kutaarifu kushindwa kuwasiliana naye. Jirani akavunja mlango na kukuta mwili huo.
Mahakamani Makin alivalia blauzi fupi nyeusi na puleki ya rangi ya shaba, koti la kijeshi la rangi ya kijani, sendo za kijivu, begi ya pinki. Alizungumza kuthibitisha jina lake na kukiri kosa katika mashitaka yake.
Makin hakuhudhuria mazishi ya Chloe katika Kanisa Katoliki la Mt. Joseph mjini Bury mwezi Aprili katika misa iliyochukua saa nzima ambapo binti huyo alitajwa kama 'malkia mdogo.'
Campbell kutoka Bury, alitozwa faini ya Pauni za Uingereza 1,050 pamoja na gharama za Pauni za Uingereza 1,175 Juni mwaka jana baada ya kukiri makosa saba ya kuvujisha taarifa chini ya Sheria ya Udhibiti Taarifa na kuamriwa kushughulikiwa kwa mashitaka mengine 22 dhidi yake.
No comments:
Post a Comment