ATEKETEA KWA MOTO HADI KUFA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI...

Mwanamke ameteketea moto hadi kufa kwenye kiti cha mbele cha gari lake lililokuwa limeharibika kugongwa na gari aina ya Porsche 4x4 kwenye barabara kuu.
Gari la mwanamke huyo aina ya Nissan Almera lilitupwa umbali wa futi 150 kando ya barabara ya M40 na kisha kulipuka moto mkubwa.
Mashahidi kadhaa walibaki wakimtazama mwanamke huyo ambaye anaaminika kuwa na umri wa miaka 60 akiteketea bila kutoa msaada wowote kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka.
Mmoja wa walioshuhudia alisema: "Gari hilo lilikuwa jeusi kabisa na ilikuwa vigumu sana kupona.
"Lilikuwa eneo la maangamizi na huzuni kubwa kwamba kuna mtu kapoteza maisha yake."
Mwingine aliandika katika mtandao wa Twitter: Ajali kubwa sana kwenye Barabara ya M40 kurejea mjini London. Mtu mmoja kapoteza maisha kwa kuteketea moto huku akijiona."
Msemaji wa Polisi wa Thames Valley alisema maofisa watahitaji kutumia kumbukumbu za mpangilio wa meno kutambua mwili wa mtu aliyeteketea kabisa kwa moto.
Mwanamke huyo ambaye alikuwa akisafiri peke yake, inaonekana aliharibikiwa gari lake kwenye upande wa kusini ambao hutumiwa na magari ya mizigo jirani na Beaconsfield, mjini Buckinghamshire majira ya saa 4:00 asubuhi. Gari lake lilipunguza mwendo na kisha kusimama katikati ya barabara ndipo likagongwa na Porsche Cayenne.
Polisi wamesema dereva wa gari la pili, amwenye miaka 47 alikimbizwa hospitali kwa matibabu ya majeraha madogo aliyopata.
"Aliruhusiwa na madaktari na anashikiliwa kwa tuhuma za kusababisha kifo kutokana na uendeshaji mbovu wa gari," msemaji huyo alithibitisha.
Askari wa kikosi cha Zimamoto waliweka uzio mbele ya Nissan katika eneo hilo kuzuia uwezekano wa madereva wengine kusababisha ajali huku wakiendelea kuondoa mabaki ya gari la mwanamke huyo.
Njia zote nne za barabara ya M40 upande wa kusini kati ya njiapanda 2 na 3 zilifungwa kufuatia ajali hiyo, na kusababisha msongamano mkubwa. Njia hiyo ilifungwa kwa muda hadi saa 10 jioni.
Polisi wa Thames Valley wameomba taarifa zaidi kuhusiana na ajali hiyo jana.
Msemaji wa Polisi alisema: "Maofisa wangependa kusikia kutoka kwa yeyote aliyeshuhudia tukio hili na pia uendeshaji wa gari kabla halijaharibika katikati ya barabara kuu."
Wanaharakati mwezi uliopita walitaka kutazamwa upya kwa sera za usalama kufuatia ongezeko kubwa la ajali za barabarani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane.
Idadi ya ajali mbaya za barabarani zimeongezeka kwa asilimia 3 kufikia 1,901 mwaka jana ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2003.
Jumla ya watu waliokufa ama kujeruhiwa vibaya imepanda kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994 hadi kufikia 25,023.
Wataalamu wa Usalama Barabarani walisema ahadi ya Serikali kumaliza 'vita kwenye vyombo vya moto' inatakiwa kubeba sehemu ya lawama, huku ikikata bajeti kwa polisi, usalama barabarani na kamera za kudhibiti madereva waendeshao kasi.

No comments: