ANUSURIKA KIFO, APOTEZA VIDOLE VYOTE MIKONONI KWA KUNG'ATWA NA PAKA...

Mtu mmoja mwenye miaka 59 ametoka hospitali baada ya kukaa huko kwa mwezi mzima katika kitengo cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalumu kufuatia madhara ya sumu katika kidonda.
Paul Gaylord, alipata madhara hayo baada ya kung'atwa na paka aliyeokotwa mitaani na kuanza kufugwa na familia yake.
Paka huyo analiyepewa jina la Charlie, alimkamata panya kisha akanasa kwenye koo lake. Inadhaniwa kuwa panya alikuwa ameathirika kwa viroboto waliobeba vimelea vya maradhi.
Mwanzoni, Paul alidhaniwa kuwa na ugonjwa wa mafua wakati alipopatwa na homa baada ya kung'atwa.
Baada ya dawa za kuua sumu kushindwa kumletea nafuu, alikimbizwa hospitali baada ya vinundu vya limfu kukua kwa kasi hadi kufikia ukubwa wa malimao.
Bado anatakiwa kufanyiwa upasuaji kuondoa vidole vyake vyeusi vilivyonyauka na vidole vya mguuni, moja ya dalili za maradhi hatari ambayo yamebatizwa jina la 'kifo cheusi'.
Japo mfanyakazi huyo wa uchomeleaji vyuma hatoweza tena kufanya kazi, ana bahati kuendelea kuwa hai.
"Wananieleza kuwa naendelea vizuri kufuatia hapa nilipofikia," alieleza akiwa kitandani kwenye Hospitali ya Kituo cha Afya cha Mt. Charles iliyopo huko Bend, mjini Oregon.
"Ninajihisi mwenye bahati. Nina safari ndefu sana lakini angalau nimemaliza moja."
Mama wa Paul, Almeda mwenye miaka 83, alielezea jinsi mtoto wake alivyokaribia mauti.
"Moyo wake ulisimama. Mapafu yake yakafa. Walitueleza hawawezi kumnusuru," alisema.
Paul alitumia karibu mwezi mzima akiwa kwenye mashine ya kupumulia, na ilifikia wakati mtoto wake wa kiume' Jake akalazimika kupanda ndege kutoka Austin, mjini Texas kuja kumuaga baba yake.
Mkewe alifanya mipango ya ubatizo kama ambavyo Paul siku zote amekuwa akijutia kutokana na kukosa fursa hiyo wakati wa utotoni.
"Niliweweseka," alisema Paul akikumbukia mwezi aliotumia akiwa chumba cha mahututi.
"Mambo yalionekana kutokwenda sawa. Saa ilikwenda kinyume."
Sasa amepata nafuu, Paul atatakiwa kujifunza upya jinsi ya kutembea na kutumia mikono yake isiyokuwa na vidole.
"Litakuwa darasa la muda mrefu," alisema. "Nitatakiwa kujifunza tena kufanya kila kitu."
Ingawa maradhi hayo kwa kawaida huwapata watu wenye rika la kati, Paul ni mtu wa 17 kuugua maradhi hayo mjini Oregon tangu mwaka 1934.
Inasababisha maambukizi yanayoua seli, kusababisha kuoza sehemu ya mwili kwa kukosa damu ambayo hupelekea wakati mwingine kukatwa viungo, kama sio kifo.

No comments: