AKUTWA AMEKUFA KWA KUCHOMWA KISU AKIWA DISKO...

Muuaji amekuwa akisakwa na polisi usiku wa kuamkia kufuatia kumvamia kijana mmoja katika klabu ya usiku na kumchoma kisu kwenye moyo bila mtu yeyote kugundua.
Jordan Malutshi mwenye miaka 17 kutoka London, alichomwa kisu mapema alfajiri akiwa kwenye sherehe katika Baa ya Face huko Mtaa wa Chatham, Reading, Berkshire.
Eneo lilikuwa na watu kibao waliokuwa wakijirusha miondoko ya R&B, ambako DJ wa Kituo cha Radio 1 Extra, Young Lion alikuwa akipigisha disko.
Washerehekeaji walisema hawakujua kabisa kama kuna mtu amechomwa kisu, wakiongeza kwamba hakukuwa na fujo zozote au mapigano wakati huo kabla Jordan hajauawa.
Mwanamke mmoja aligundua damu kwenye nguo yake na kumweleza mfanyakazi wa baa hiyo akiwa hajui ilikotokea.
Jordan alikutwa amelala sakafuni karibu na vyoo vya klabu hiyo muda mfupi baadaye.
Polisi waliitwa klabuni hapo majira ya Saa 9:50 alfajiri kujaribu kuokoa uhai wake eneo la tukio kabla ya kupelekwa hospitali.
Lakini alifariki kutokana na majeraha yake muda mfupi baada ya kupokelewa katika Hospitali ya Royal Berkshire, polisi wa Thames Valley wamesema.
Taarifa za uhalifu zimefikia kwenye mauaji
Mkuu wa Upelelezi Inspekta Kevin Mahon, wa vikosi vya Kitengo cha Makosa Makubwa ya Jinai, alisema: "Hili lilikuwa tukio la kipekee ambapo kijana alipoteza maisha yake bila hatia.
"Tumeunda timu ya wapelelezi inayofanya kazi kuhusiana na kesi hii na kuwajibika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio yaliyopelekea tukio hili la msiba.
"Tunajua kulikuwa na idadi kubwa ya watu kwenye Baa ya Face wakati wa tukio hilo na ninaomba yeyote aliyeshuhudia, au mwenye taarifa zozote ambazo zitatusaidia katika uchunguzi wetu kutupigia simu."
Uchunguzi wa mwili uliofanyika umegundua kifo chake kimesababishwa na jeraha katika moyo lililotokana na kuchoma na kitu chenye ncha kali.

No comments: