Abiria mwenye njaa amenaswa na kamera akisababisha hasara ya Pauni za Uingereza 200 kwenye basi kwa kutafuna kiti chake.
Picha zilizonaswa na kamera za CCTV zimesambazwa zikimuonesha mtu ambaye hajafahamika akitafuna kiti cha basi namba 12 katika eneo la Torbay mjini Devon.
Mtu huyo, mwenye nywele nyeusi na mwili wa wastani, alikuwa kwenye basi kwa takribani dakika 20 kabla ya kuanza kujipatia mlo wake usiokuwa wa kawaida.
Ofisa wa Polisi Gary Blee wa Kituo cha Polisi cha Torbay alisema: "Mtuhumiwa huyo mwanaume alipanda basi Namba 12 huko Paignton na alitafuna kiti alichokuwa amekalia ambapo alisababisha hasara ya Pauni 200."
Kisha akaendelea kuvuta ngozi ya kiti hicho kwa mikono yake na hivyo kuongeza ukubwa wa tundu.
Polisi wamewaomba mashuhuda wa tukio hilo ambalo lilitokea Mei 25, mwaka huu majira ya Saa 2 asubuhi, kufika kutoa ushahidi.
Msemaji wa kampuni ya mabasi ya Stagecoach alisema: "Kwa kawaida hilo sio tukio kubwa kwa maana ya hasara iliyosababishwa, lakini si la kawaida.
"Tunashirikiana na polisi na kuwasaidia wanachohitaji katika uchunguzi wao."
Masharti ya uchukuzi ya Stagecoach yanawaamuru abiria: "Kuepuka kubeba vyakula na vinywaji ambayo vitawasababishia kero abiria wengine au vinginevyo kusababisha uvunjaji wa sheria."
Mtu huyo pia alivunja sheria kwamba abiria hatakiwi 'kwa makusudi kuharibu au kufuja sehemu yoyote ya gari."

No comments:
Post a Comment