AANGUKA NA KUFA KORTINI BAADA YA UONGO WAKE KUGUNDULIKA...

Chumba cha mahakama kiliingia hofu pale mwanaume ambaye muda mfupi uliopita alitiwa hatiani kwa uchomaji nyumba yake yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3.5 kuanguka na kufariki mbele yao.
Michael Marin mwenye miaka 53 alikutwa na hatia ya uchomaji mali kwa makusudi na baraza la wazee wa mahakama kwenye Mahakama Kuu ya Maricopa County. alionekana kushitushwa na kufumba macho yake wakati hukumu ikisomwa kabla ya kuweka kitu mdomoni na kuosha kwa kimiminika kilichokuwa ndani ya chupa ya maji ya plastiki.
Katika video ya kushitua iliyopigwa kwenye chumba cha mahakama, kisha alianguka sakafuni dakika chache baadaye katika misukosuko. Marin alikimbizwa hospitalini mjini Phoenix, Arizona, ambako alitangazwa kufariki dunia.
Wakati mashitaka dhidi ya Marin yalipoanza Mei, waendesha mashitaka walisema anaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 16 jela kama akikutwa na hatia.
Marin alichoma nyumba yake iliyoko Phoenix Julai 5, 2009 baada ya kushindwa kuiuza katika mnada wa hadhara.
Wachunguzi wa Kitengo cha Moto wamegundua kwamba moto huo uliwashwa kwa kukusudia baada ya kukuta vitu kadhaa vikiwa mahali pake wakati moto huo ukisambaa katika nyumba hiyo yenye eneo la Futi za Mraba 6,600 pamoja na gereji nne.
Marin baadaye aliziambia mamlaka husika kwamba aliokoka kutoka kwenye moto huo baada ya kukwea kwa kamba kutoka ghorofa ya pili na kuvalia suti maalumu ya kuogelea.
Hakuna aliyejeruhiwa kwenye moto huo lakini mashitaka yanamhusisha na uchomaji mali kwa makusudi na hivyo kukabiliwa na kifungo cha miaka hiyo gerezani mjini Arizona.
Waendesha mashitaka wamedai Marin alichoma nyumba yake katika kukata tamaa sababu hakuweza tean kulipia mkopo wake wa nyumba.
Uchunguzi kuhusu matumizi ya dawa za kulevya utafuatia dhidi ya mwili wa mtu huyo mwenye miaka 53 sambamba na chupa ya maji aliyokunywa.
Marin, baba wa watoto wanne na babu wa wajukuu wawili, alisoma kwenye Shule ya Sheria ya Yale. Alikuwa mfanyabiashara wa mitaani ambaye alikuwa akiuza michoro ya msanii Pablo Picasso na kujipambanua magazetini kama "Msakaji Msisimko Makini" baada ya kupanda Mlima Everest na safari zake kwenye misitu minene ya kusini-mashariki mwa Asia.

No comments: