Pengine sasa Wahehe ama maarufu kama 'Wanyalukolo' watapata nafuu kidogo baada ya kusoma habari hii ya picha zinazokera zikionesha mbwa wakipikwa na kugawiwa kama mlo katika utamaduni mgumu wa Kichina.
Wanyama hao wamekatwa vipande vidogo na kupikwa mbele ya walaji licha ya kushamiri kwa kampeni ya kupinga ukatili.
Kundi la wanaharakati wa Kichina mjini Yulin, katika jimbo la Guangxi, wavamia soko la nyama ya mbwa wakiendesha kampeni dhidi ya ulaji wanyama hao.
Msanii Pian Shan Kong alipiga magoti mbele ya miili ya wanyama hao akitubu kwa dhambi za watu wakati akikiri kwa wanyama hao waliokufa wakati wa maandamano.
China bado haijatangaza rasmi ukatili dhidi ya wanyama kuwa ni kinyume cha sheria na kusitisha utamaduni mgumu licha ya kampeni zinazoendeshwa na wanaharakati wa haki za wanyama.
Umoja wa wapenda wanyama umechipuka kwenye miji mbalimbali ya China katika miaka ya hivi karibuni.
Wakati Wachina wengi wakifurahia wingi wa nyama ya mbwa, hususani wakati wa majira ya baridi, baadhi wanapinga zoezi la kupiga mbwa hadi kufa katika baadhi ya miji kuondoa damu katika nyama.
Wakati chakula kinapoadimika, mbwa wanaliwa kama chakula cha dharura kote China katika zoezi linaloonekana kama limekubalika kwa jamii.
Wakati nchi ikiwa kijito zaidi, ongezeko la ukubwa wa familia zinazonunua mbwa kwa ajili ya kufuga linachochea ukuaji wa kampeni dhidi ya ukatili kwa wanyama.
Mwezi Aprili, zaidi ya mbwa 500 waliopangwa kuuawa waliokolewa pale lori walimokuwa wamebebwa kupelekwa kwenye nyumba ya mauaji lilipokamatwa na wanaharakati.
Wengi wa viumbe hao 505 wamenusurika katika mpango huo, wakiwa katika hali mbaya na ukosefu wa maji wakati wote wa safari yao ya karibu maili 1,000 kwa njia ya barabara.
Lakini wokovu ukatokea ukiwa umechelewa mno kwa mbwa 11 ambao walikuwa taabani kwa ukosefu wa maji na mrundikano.
No comments:
Post a Comment