Mabao mawili maridadi ya kipindi cha kwanza yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji 'mtukutu' Mario Balotelli usiku wa kuamkia leo yaliiwezesha timu yake ya taifa ya Italia "The Azzuri" kutinga fainali ya Michuano ya Ulaya "Euro 2012" kwa kuibwaga Ujerumani kwa mabao 2-1. Bao la kufutia machozi la Ujerumani katika mechi hiyo lilifungwa na Mesut Ozil kwa njia ya penalti kipindi cha pili. Kwa matokeo hayo, Italia sasa itakutana na mabingwa watetezi Hispania katika mechi ya fainali siku ya Jumapili. Pata utamu wa mabo hayo kwenye video hapo juu.
No comments:
Post a Comment