JINSI FREEMASONS WALIVYOENEA KUTOKA UINGEREZA HADI MAREKANI...

Kutoka wakati watu walipokuwa wakisafiri kwa farasi, na meli zinazotumia matanga, u-Masons uliienea kwa kasi ya kushangaza.
Hadi kufikia kwaka 1731, wakati Benjamin Franklin alipojiunga na u-Masons, kulikuwa na majumba kadhaa ya kukutania katika makoloni, na huko u-Freemasons ulieenea kwa kasi kubwa wakati huo Marekani ikionekana kama inazidi kwa kuelekea magharibi.
Mbali na Franklin, wengi wa waanzilishi - kama George Washington, Paul Revere, Joseph Warren, na John Hancock - walikuwa wa-Masons.
Wamasons na U-Freemasons ulitoa mchango muhimu sana katika Vita ya Mapinduzi na pia kutoa mchango muhimu katika utaratibu wa kawaida wa katiba na midahalo inayoizunguka uidhinishaji wa Muswada wa Sheria.
Mingi ya midahalo hiyo ilikuwa ikifanyika katika nyumba Wamasons walikokuwa wakikutania.
SEHEMU WANAZOKUTANIA
Wanachama au wafuasi wa udugu wa u-Freemasons huwa wanakutana katika sehemu maalumu ambayo ni chumba au jengo.
U-Freemasons au majengo ya u-Masons wakati mwingine huitwa 'Mahekalu', kwa sababu sehemu kubwa ya alama za ishara na masomo ya ki-Freemasons walikuwa wakifundishana katika majengo ya Hekalu na Mfalme Suleiman katika Nchi Takatifu.
Hayo ni majengo yaliyojengwa na mafundi waashi kandokando ya makanisa wakati wa kujengwa.
Wakati wa baridi, wakati mafundi waashi waliposimamisha ujenzi, walikuwa wakiishi katika sehemu hizi walizokuwa wakikutania wale wa-Masons na kuendelea na kazi za kutia mawe nakshi.
Kama uliwahi kuangalia taarifa za C-Span zinazotolewa na Bunge la Mamwinyi la London, utagundua kuwa ramani yake inafanana.
Kwa vile u-Freemasons umeenezwa Marekani ukitokea Uingereza, bado tunatumia ramani za ujengaji wa Kiingereza, na hata kutumia vyeo vya Kiingereza kwa maofisa wake.
Mstahiki Mkuu wa Nyumba hizo alikuwa akikaa upande wa Mashariki. Neno 'Mstahiki' linatumiwa likiwa na heshima ile ile kama 'Mheshimiwa'.
Huwa anaitwa Mkuu wa Nyumba kwa maana ile ile kama vile kiongozi wa kundi la onyesho la muziki anavyoitwa 'Mkubwa wa Onyesho'. Ni utaratibu wa kisheria kwa 'Kiongozi'.
Katika taasisi nyingine angeweza hata kuitwa 'Rais'. Waangalizi wakubwa na wadogo ni 'Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais.
Mashemasi ni matarishi, na wengine ni wahudumu wengine wanaoshughulika na vinywaji. Kila nyumba ina madhabahu inayohifadhi 'Kitabu cha Sheria Takatifu.'
Nchini Marekani na Canada lazima kuwe na Biblia katika nyumba hizo.
JE, U-FREEMASONS NI ELIMU?
Hapana shaka, kwa maana halisi elimu ndiyo kiini cha u-Freemasons. Tumesisitiza umuhimu wake kwa muda mrefu sana.
Tukirudi nyuma katika Zama za Kati, shule zilikuwa zikiendeshwa katika nyumba zilizojengwa kwa mawe na mafundi waashi. Unatakiwa ujue zaidi jinsi ya kujenga kanisa - elimu ya jiometri, uhandisi ujenzi na hesabu, kwa kuanzia.
Na wakati ule elimu haikuwa pana sana. Elimu ya shule za kawaida na vyuo vilikuwa vikifundisha watu kazi mbalimbali makanisani au masomo ya sheria au dawa. Na ulitakiwa kuwa mmoja wa watu wa daraja la juu ili kupata nafasi katika shule hizo.
Na u-Freemasons huunga mkono maendeleo ya elimu na kujenga uweledi kwa wanachama wao, wakisisitiza kuwa kujifunza zaidi kuhusu mambo mengi ni muhimu kwa mtu yeyote kuwa na akili changamfu.

U-Freemasons hufundisha baadhi ya kanuni muhimu. Hakuna kitu cha kushangaza sana katika orodha ya vitu wanavyofundisha. U-Freemasons hufundisha kwamba: Kwa vile Mungu ndiyo Muumba, watu wote ni wana wa Mungu.
Kwa sababu hiyo, wanaume wote na wanawake ni kama kaka na dada, wanaostahili heshima, waheshimiwe maoni yao, na kutilia maanani hisia zao. Kila mtu abebe jukumu la maisha yake mwenyewe na matendo yake.
Si masikini wala matajiri, si walio na elimu wala wasio nayo, si wenye afya wala wagonjwa haiwi sababu ya mtu kutomfanya mtu kutenda jambo jema analoweza kufanya.
Hakuna mtu mwenye haki ya kumwambia mtu mwingine kitu cha kufanya au kuamini. Kila mtu ana haki kuwa uhuru kamili wa kiueledi, kiroho, kiuchumi na kisiasa.
Hii ni haki iliyotolewa na Mungu, haikutolewa na mtu.
Uonevu wa namna yoyote ni kinyume cha sheria.
Kila mtu lazima ajifunze na kuwa ni msimamizi wake mwenyewe.

Kila mtu lazima ahakikishe kuwa hali yake ya kiroho inashinda majaribu yasiyo ya kibinadamu. Kwa maneno mengine kama mtu akikasirishwa hatakiwi kufanya vurugu.
Hata kama mtu atakuwa na tabia ya uchoyo, analazimka kuwa na huruma. Hata kama tunataka 'kumuondoa' mtu au kumfuta kazi ni lazima tukumbuke kuwa yeye ni binadamu na anastahili heshima kutoka kwetu.
Hata kama tuko katika hali ya kukata tamaa lazima tujipe moyo. Hata kama kuna watu wanatuchukia, sisi lazima tuonyeshe upendo na wala si nasi kuwachukia, japo si kitu rahisi!
MASHARTI YA KUJIUNGA NA FREEMASONS
Mtu anayetaka kujiunga na u-Freemasons lazima awe ni (mtu aliyemo katika udugu), aliyekamilika kimwili na kiroho, anayeamini Mungu kwamba ndiye mtendaji wa yote, awe na umri wa chini unaokubalika na wa-Masons katika nchi yake, na awe na tabia nzuri.
(Kwa bahati nzuri tunapozungumzia sharti la 'aliyekamilika kimwili' - inayotokana na mafundi wa uashi katika Zama za Kati - haina maana kuwa mtu wa kawaida hawezi kuwa m-Masons. Wapo wengi wa aina hiyo).
Hayo ndiyo masharti ya kawaida kwa mtu kuweza kujiunga na wa-Freemasons.
Lakini kuna masharti mengine yasiyo ya kawaida. Anayetaka kujiunga na wa-Masons lazime aamini katika kuwasaidia wengine. Lazima aamini kuwa kuna maisha ya zaidi ya kuwa na furaha na fedha.
Lazima akubali kuheshimu maoni ya watu wengine. Lazima akubali kukua na kuendelea kama binadamu.
Mafundi waashi hawakuwa watu kutoka matabaka ya juu ya kiutawala. Kwa hiyo shule hizo zililazimika kufundisha habari za stadi zilizo za lazima.

Kujikita zaidi kwa u-Freemasons katika elimu kulianzia hapo na kuendelea. Ma-Freemasons walianzisha shule za kwanza za umma barani Ulaya na Marekani.
Waliunga mkono sheria ya elimu kwa wote. Katika miaka ya 1800, Wa-Masons wakiwa kama kundi, walishawishi kuanzishwa kwa mipango ya elimu iliyoungwa mkono na serikali na vyuo vilivyotokana na msaada wa ardhi iliyoidhinishwa na serikali.
'Leo hii ma-Freemasons tunalipia mamilioni ya dola kwa watu kupata elimu ya juu kila mwaka. Tunawahimiza wanachama au wafuasi wetu kujitolea muda wao katika shule za jamii, kununua mahitaji ya shule kwa walimu, kusaidia mipango ya masomo na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa kila mtu - wakubwa kwa wadogo - anapata fursa ya elimu bora kabisa.
Imani ya dini lazima iwe ndiyo kiini cha maisha yetu. Lazima imani tuionyeshe katika nyumba za ibada, na wala si kwa u-Freemasons, japo u-Freemasons mara nyingi unafundisha kwamba imani ya mtu, hata ingekuwaje, ndiyo kiini cha maisha yetu mema.

Kila mtu ana jukumu la kuwa raia mwema anayefuata sheria. Lakini hiyo haina maana hatuwezi kubadilisha mambo, lakini mabadiliko lazima yafanyike kwa njia za kisheria.
Ni muhimu kufanya kazi ili kuifanya dunia hii kuwa mahali pazuri pa sisi wote kuweza kuishi.
U-Freemasons unafundisha umuhimu wa kufanya mambo mema, si kwa sababu humuhakikishia mtu njia ya kwenda mbinguni - hilo ni suala la kidini si la udugu - lakini ni kwa sababu tuna jukumu la kufanya maisha ya kila mtu yawe ya kujitosheleza kadiri watakavyoweza. Heshima na uadilifu ni vitu vya lazima katika maisha kwani maisha bila ya vitu hivyo viwili hayana maana yoyote.
Imetafsiriwa na Bakari Omari Bakari 'Teacher' -0655 188666.
Usikose sehemu ya mwisho kesho...

2 comments:

Unknown said...

sawa hii ni sahihi na sawa,ila ni kwanini masuala yao ufanya kinyume na machukizo ya Mungu..na kama si imani ya kidini ni umoja wa kindugu basia ni kwanini wafanye yamchukizayo Mungu...?
naomba kufahamu je hawa mafreemasonia hawamwamini Mungu.

Unknown said...

sawa hii ni sahihi na sawa,ila ni kwanini masuala yao ufanya kinyume na machukizo ya Mungu..na kama si imani ya kidini ni umoja wa kindugu basia ni kwanini wafanye yamchukizayo Mungu...?
naomba kufahamu je hawa mafreemasonia hawamwamini Mungu.