CHEKA TARATIBU...

Balozi mmoja hapa nchini baada ya kumaliza muda wake akarejea kwao. Mara baada ya kufika huko akaonana na Balozi mpya ambaye alikuwa akijiandaa kuja Tanzania kuchukua nafasi yake. Katika mambo mengi waliyoongea, yule Balozi mpya akauliza, "Nini ulichojifunza kwa watu wa Tanzania?" Balozi wa zamani akajibu, "Wanapoulizwa swali nao huuliza swali hapohapo kabla ya kutoa jibu." Duh, yule Balozi mpya hakuelewa wala hakutaka kuamini mpaka aje kuthibitisha mwenyewe akifika. Siku ya safari ikawadia na Balozi yule mpya akawasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na kupokelewa na Waziri mmoja. Bila kupoteza wakati baada ya kusalimiana akauliza, "Hivi ni kweli Tanzania mna tabia mnapoulizwa swali na nyie huuliza swali badala ya kutoa jibu?" Yule waziri akacheeka na kisha kujibu, "We nani kakwambia habari hizo?" Hapo balozi akashangaa sana na kumpigia simu mwenzake kuthibitisha hilo...

No comments: