UVUMILIVU WAKE UMEMSABABISHIA SASA AWE KIPOFU...

KUSHOTO: Tina kabla ya tukio (juu) na alivyo sasa. Callous Shane Jenkin (chini). KULIA: Tina Nash akiongozwa na polisi kuingia mahakamani jana.
Mama ambaye alitobolewa macho na mpenzi wake, jana amebainisha kwamba jambo linalomuumiza moyo kwa sasa ni ukweli kuwa hawezi tena kuona sura za watoto wake.
Shane Jenkin mwenye miaka 33, mwenye rekodi ya ghasia alimshambulia mama wa watoto wawili, Tina Nash katika shambulio lililodumu kwa masaa 12 nyumbani kwake kitongoji cha Hayle, Cornwall, likimwacha mwanamke huyo mwenye mvuto akiwa kipofu kabisa.
Wapasuaji walilazimika kuondoa jicho lake moja na kushindwa kabisa kuokoa jingine, baada shambulio hilo ambalo pia lilimwacha Tina akizirai huku akiwa amevunjika taya lake la kushoto na pua yake, Mahakama ya Truro Crown ilielezwa.
Callous Shane Jenkin ndiye alikuwa chanzo cha ugomvi huo na amekuwa akitumikia adhabu ya kutokwenda baa kwa miaka mitano kufuatia vurugu zake.
Alizuiwa kushiriki baa mwaka 2010 kufuatia kumpiga polisi, mlinzi wa baa mwenyekiti alieleza na mhudumu wa baa ya Penzance akisema Jenkin aliwahi kujaribu kunyofoa macho ya mwanaume mmoja siku za nyuma katika ugomvi.
Tina alipigwa picha kwa mara ya kwanza jana tangu lilipotokea shambulio hilo, baada ya kuhudhuria shauri mwaka akiwa amejificha kwa miwani ya jua mikubwa myeusi.
Katika taarifa iliyotolewa hadharani baada ya Jenkin kukiri kosa mbele ya mahakama jana, Tina alisema kuwa ana furaha sababu Jenkin 'amekubali kuwajibika kwa kubadili maisha yake milele'.
Alisema: "Nadhani kitu kigumu ni ukweli kwamba sitaweza tena kuona sura za wanangu." Watoto wake wa kiume wenye miaka 13 na mwingine mitatu kwa sasa, walikuwa nyumbani hapo usiku ambao lilitokea shambulio hilo.
"Hakika nadhani kama wanangu wasingekuwapo nyumbani usiku ule, nadhani nisingekuwa hapa," aliongeza.
"Amechukua kila kitu kutoka kwangu na amenipora kitu cha thamani sana maishani mwangu - kuona."
"Nakosa vitu ambavyo watu huviona kwa nadra kama kuona anga na bahari.
"Hakina nahisi hivyo, pale aliponivamia, alikuwa amedhamiria kuniua."
Jenkin, ambaye amejengeka vizuri misuli anayeishi kitongoji cha Hayle, Cornwall, alishitakiwa kwa jaribio la kuua na amekiri mahakamani leo. Atahukumiwa mwezi ujao mbele ya uwepo wa wataalamu wa magonjwa ya akili.
Nje ya Mahakama, Inspekta wa Polisi Chris Strickland anayeshughulika na vitongoji vya Devon na Cornwall alisema kesi hiyo ilikuwa ngumu kuwahi kuwahi kushughulikia katika maisha yake.
Tina ambaye alipambana kishujaa na Jenkin mahakamani wakati wa kusikilizwa shauri hilo siku zilizopita, alisema anajihisi 'kazikwa akiwa hai, na kutolewa kwenye umiliki wa maisha yake' kutokana na shambulio hilo.
Mdhalilishaji Jenkin amekuwa akimpiga mama huyo hapo kabla, lakini Tina amekuwa akimtetea na kusaidia kumtoa jela.
Mwanamke huyo aliyejawa hofu ameonya waathirika wa ugomvi majumbani 'kuondoka mara moja kabla hawajachelewa', akitolea mfano wake kwamba alidhani angeweza kumbadili mpenzi wake huyo badala yake akazidi kubadilika.
"Nilikuwa natarajia kwenda kulala sababu katika fikra zangu nilijua naona. Ilikuwa pale nilipoamka ndipo ukweli ukajulikana," anasema.
"Siku nyingine sitaki kabisa kuamka lakini natakiwa kuwaonyesha hatima yao wanangu na hii ni changamoto yangu."
Akiongeza kwenye mahojiano na BBC, Tina alisema: "Najihisi kama mzimu. Naweza kuwasikia wote walionizunguka, lakini nashindwa kuona japo mkono wangu mbele ya uso wangu."
Mwanamke huyo mwenye miaka 32 anakiri kuwa kujiamini kwake kumetoweka na hajui anaonekanaje baada ya kupoteza macho yake.
"Huyu sio mimi," aliongeza. "Natamani kuona dunia, ninakosa kila kitu."
Alisema kwamba Jenkin alifoka kwa sauti akimshutumu kuwa shambulio hilo kalitaka mwenyewe huku akiwa anagaagaa sakafu akichuruzika damu na maumivu nyumbani kwake.
Tina anasema haelewi anawezaje kumdhuru hivyo mtu anayemhudumia, na kwamba kamwe hawezi kumsamehe kwa kumtelekeza baada ya kumshambulia.
Tina aliruhusiwa kutoka hospitali kabla ya siku yake ya kuzaliwa mwaka jana, na kuanza kujifunza kutembea bila kuona.

1 comment:

Anonymous said...



My web sitŠµ; tantric massage in London
Stop by my blog ; erotic massage