MAMA WA WHITNEY AHUZUNISHWA NA RIPOTI YA KIFO CHA MWANAE...

Whitney Houston wakifurahi na mama yake, Cissy wakati wa uhai wake.
Mama mzazi wa Whitney Houston amehuzunishwa na ripoti ya uchunguzi wa kifo cha binti yake iliyosema kuwa mwimbaji huyo wa zamani alitumia kiwango kikubwa sana cha dawa za kulevya muda mfupi kabla ya kifo chake.
Cissy Houston amewaeleza marafiki zake wa karibu kwamba alilia sana aliposikia kwa mara ya kwanza ripoti ya uchunguzi kwamba umekutwa unga (ambao baada ya vipimo ulibainika kuwa ni dawa za kulevya aina ya cocaine), kijiko kinachotumika kuchomea dawa hizo ndani ya chumba hicho.
Cissy ameweka bayana hofu yake kwamba watu watamkumbuka Whitney kama 'teja' badala ya mwimbaji mahiri mwenye kipaji na mama wa familia.
Mama huyo alikumbushia moja ya maonyesho bora ya Whitney mwaka 1991 pale alipoimba kwa ustadi mkubwa wimbo wa taifa.
"Hivi ndio vitu ambavyo watu wanatakiwa kutumia katika kumkumbuka Whitney."

No comments: