NDIVYO TULIVYO...

 IMEANDIKWA KWA KISWAHILI!!  Lakini jambo ambalo pengine halishangazi sana kwa utamaduni wa wakazi wa Dar es Salaam, dampo dogo likiwa limechipuka kuzunguka kibao cha Ilani kinachokataza utupaji wa taka eneo hilo. Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni naamini kabisa wanapita na kuona hali hii. Ndio maana nashawishika kuamini NDIVYO TULIVYO!
 KAMA HATUKUJIPANGA TUSUBIRI!!  Barabara inayopita nyuma ya kituo cha mafuta cha Mwanamboka eneo la Kinondoni Studio ikiwa imetelekezwa baada ya kuchimbwa chimbwa kwa mbwembwe na watu wanaoaminika kuwa ni wakandarasi kutoka Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka. Awali barabara hii ilikuwa ikipitika bila shida, lakini baada ya watu hao kufanya 'madudu' na kuitelekeza imekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo hasa wakati wa mvua. (Picha zote na ziro99blog).

No comments: