CHEKA TARATIBU...

Kikundi cha madaktari kimekaa kikao kujadili mustakabali wao kazini. Wanne kati yao wakaamua kubwaga manyanga na kutoka nje ya kikao kwa wakati mmoja. Wakiwa nje dokta wa kwanza akasema, "Kila mara watu wanatufuata na shida zao tuwatatulie, lakini sisi hatuna wa kumpelekea shida zetu." Wote wakamuunga mkono kwa hoja yake hiyo. Dokta wa pili akasema, "Kwakuwa sisi ni wataalamu, kwanini tusitumie muda huu kusema shida zetu tutatuliane wenyewe?" Wote wakaafiki. Dokta wa kwanza akaanza kupasua lililo moyoni mwake, "Mwenzenu dhamira yangu siku zote ni kuua mgonjwa wangu." Dokta wa pili naye akalonga, "Napenda sana vitu vya gharama kiasi cha kufanya kila mbinu kuwarubuni wagonjwa wangu ili tu nipate pesa za kununulia vitu nitakavyo." Dokta wa tatu akatoboa siri yake, "Nimekuwa nikijihusisha na wizi wa dawa na kuwatuma wagonjwa wangu kuziuza." Dokta wa nne akamalizia la kwake, "Najua sitakiwi kufanya hivi, lakini bila kujali ugumu wake, ni kwamba siwezi kutunza siri hizi..."

No comments: