CHEKA TARATIBU...
Jamaa mmoja baada ya kushuka kwenye basi maeneo ya Kinondoni Makaburini kaamua kupita njia ya mkato kwenda kwake majira ya saa saba za usiku. Akiwa katikati ya giza nene, akasikia sauti za vibaka kwa nyuma yake zikimwamuru kupiga magoti na kusalimisha kila alichokuwa nacho huku wakiparuza mapanga yao chini. Haraka jamaa akapata akili ya kutimua mbio, ndipo wale vibaka walipoanza kumfukuza. Baada kama ya dakika kumi huku jamaa akiwa kaanza kuchoka, limkamjia wazo la kujificha katika makaburi ya jirani. Kutokana na giza nene, wale jamaa wakapita bila kumwona. Lakini hatua kadhaa mmoja wao akawaambia wenzake, "Hataa, huyu hajaenda mbali lazima kajificha humu humu." Wakajigawa na kuanza kumsaka mle makaburini. Jamaa kuona hivyo akaamua kuvua nguo zake zote na kukaa juu ya moja ya makaburi. Punde akawaona wale vibaka wakimjia na kusimama mbele yake na mapanga mkononi. "Ebwana umemuona mtu kapita spidi hapa?" Yule jamaa kwa akili za haraka akawajibu, "Mie hapa mgeni, nimezikwa jana tu, na hapa napunga upepo labda jaribuni kuwauliza hao hapo ndio wenyeji," alisema huku akinyooshea makaburi mengine. Wale vibaka kusikia hivyo wacha watimue mbio kila mmoja na njia yake!! Duh...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment