ARSENAL KAMA YANGA...

Mabao safi yaliyofungwa kipindi cha kwanza na Laurent Koscienly, Tomas Rosicky na Robin van Persie hayakutosha kuivusha Arsenal kuelekea hatua nyingine wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 Bora dhidi ya AC Milan kwenye Uwanja wa Emirates usiku wa kuamkia leo. Matokeo hayo yanakamilisha ule usemi wa "Umekumbuka shuka asubuhi" kufuatia kuvurunda katika mechi ya kwanza iliyofanyika nchini Italia wiki mbili zilizopita ambapo Washika Mitutu hao wa london walikubali kichapo cha mabao 4-0. Sasa Arsenal kama Yanga tu, kwani sasa imebakiza matumaini yake kwenye Ligi Kuu ya England pekee. Yanga ya Tanzania nayo imetolewa na Zamalek ya Misri kwenye Klabu bingwa Afrika na kuelekeza nguvu kwenye Ligi Kuu ya Bara!!

No comments: