Treni ya Shirika la Reli ikiwasili Stesheni ya Mwanza. |
Wizara ya Uchukuzi, imebainisha wazi kuwa hali ya kifedha ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) si nzuri kiasi cha kushindwa hata kukarabati kwa muda mrefu vituo vyake ambavyo kwa sasa vina hali mbaya.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati (CCM).
Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua ni lini TRL itajenga tangi la maji kwenye kijiji cha Hika ili wananchi wa eneo hilo waweze kupata maji.
Pia alitaka kujua kuwa ni lini wananchi wa Hika watalipwa fidia na Serikali kwa kuwa ndio wanaolinda chanzo cha maji kinachotumiwa na shirika hilo.
“Je, TRL na Wizara zitakuwa tayari kushirikiana na wananchi wa Saranda kwa ajili ya kujenga vibanda vizuri vya chakula ili kuimarisha ajira ya watu wa Saranda na wasafiri wapate mahala pazuri pa chakula?” Alihoji.
Akijibu swali hilo, Dk Tizeba, alikiri hali ya shirika kuwa mbaya, hivyo ni vigumu kwa sasa kuwajengea tangi wananchi wa Hika ikiwa ni pamoja na kukarabati vituo vyake vyote kuanzia Dar es Salaam, Mwanza hadi Kigoma.
Alisema programu iliyopo ya ufufuaji wa Reli ya Kati itahusisha pia kufufua vituo vyote vya treni kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma na maeneo mengine.
Kuhusu kujengwa kwa vibanda vya huduma ya chakula, alisema maeneo mengi ya vituo vya treni hayako katika hali nzuri.
Awali katika swali lake la msingi, mbunge huyo alitaka kujua ni lini mabomba hayo yatakarabatiwa ili kuzuia upotevu mkubwa wa maji yanayovuja njiani.
Akijibu swali hilo, Tizeba alisema bomba la maji linaloanzia Hika kwa sasa liko katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati Novemba, mwaka jana.
Aidha, alisema TRL ina nia thabiti ya kusaidia kijiji cha Hika kutoa huduma za jamii katika sekta za elimu na afya, lakini hali ya kifedha si nzuri kutokana na utendaji wa kampuni kushuka.
“Hali hii imesababisha mapato ya kampuni kushuka kiasi cha kutokidhi gharama za uendeshaji,” alisema.
Wakati huo huo, Tanzania imeingia makubaliano na Shirika la Biashara la Canada kuboresha usafiri wa reli nchini.
Akizungumza wakati wa kusaini jana, Naibu Katibu Mkuu ambaye anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange, alisema hatua hiyo itaimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili katika usafirishaji wa reli.
“Kwa sasa usafiri wa reli unafanya kazi kidogo na tunahitaji uwekezaji mkubwa katika vichwa vya treni na mabehewa,” alisema.
Mwamunyange alisema kutokana na gharama za usafirishaji mizigo kuwa juu, kuna haja ya kuwa na mfumo imara wa reli, ili kuondoa tatizo hilo.
Alisema Serikali imefanya jitihada za kuhakikisha mfumo wa reli nchini unaimarika na kwa sasa unaendelea ukarabati wa Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam hadi Tabora.
Balozi wa Canada nchini, Alexandre Levesque alisema makubaliano hayo yataiwezesha Tanzania kupata vifaa, huduma na utaalamu kutoka Canada.
Canada imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Tanzania katika sekta ya usafirishaji. Mwaka 1972, Serikali ya Canada ilitoa vichwa vya treni 20 kwa Tanzania na kusaidia katika kukarabati na mafunzo.

No comments:
Post a Comment