| Skrini kubwa ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilivyokuwa ikisomeka mara baada ya mechi kati ya Taifa Stars na Morocco ambapo vijana wa Tanzania walifanikiwa kupiga hatua nyingine kuweza kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya pili katika kundi lake ikiwa imejikusanyia pointi 6 nyuma ya Ivory Coast yenye pointi 7. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars. |
0 件のコメント:
コメントを投稿