Jennifer Wederell |
Msichana wa Uingereza, Jennifer Wederell mwenye miaka 27 aliyekuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye kibofu, amefariki kwa saratani baada ya kuwekewa mapavu ya mvutaji mkubwa wa sigara katika zoezi la upandikizaji viungo.
Kwa mujibu wa BBC News, Jennifer alikuwa katika orodha ya wanaosubiri upandikiziwaji mapafu kwa miezi 18 tangu Aprili 2011, alipoelezwa kwamba yamepatikana mapafu yanayofanana na yake.
Alifanyiwa upandikizwaji, bila kufahamu kwamba mchangiaji huyo alikuwa mvutaji sigara. Februari 2012 madhara makubwa yaligundulika kwenye mapafu yake. Alifariki baada ya kindi kisichozidi miezi 16 baada ya kupandikizwa.
Baba yake, Colin Grannell, alisema anaamini binti yake amekufa kifo chenye maana kwa mtu mwingine zaidi.
"Mshituko ghafla ukabadilika kuwa ghadhabu wakati tahadhari zote zilielezwa saa moja kabla ya kupandikizwa," aliieleza BBC.
Suala la Jennifer linaibua masuala magumu kuhusiana na upandikizaji viungo. Aligundulika kuwa na uvimbe katika kibofu, maradhi endelevu yanayodhoofisha mapafu ambayo yamewakumba zaidi ya watu 70,000 duniani kote, kuanzia umri wa miaka miwili. Alipokuwa katika umri wa miaka 20, alitegemea mtungi wa oksijeni masaa 24 kuweka kuishi.
Je ingekuwa vema kwake kugomea upandikizwaji, na kutarajia seti ya viungo vingine kupatikana ambavyo vingefanana na aina ya kundi lake la damu na kuja kutoka kwa mtu asiyevuta sigara?
"Hapana," alisema Dk G. Alexander Patterson, mkurugenzi upasuaji wa upandikizaji wa mapafu katika kituo cha Upandikizaji cha Washington University and Barnes-Jewish mjini St. Louis, moja ya mpango mkubwa wa upandikizaji viungo katika Marekani. "Kama angekuwa anaumwa sana na kuwa na nafasi finyu ya kuishi, ilikuwa sahihi kukubali upandikizaji."
Patterson alisema hospitali karibu zote, zikiwamo za Marekani, pia zinapandikiza mapafu ya wavutaji sigara ikiwa tu yapo katika ubora mzuri.

No comments:
Post a Comment