BABU AJIPIGA KIBERITI KWA KUZIDIWA NA MADENI...

Babu amejiwasha moto mwenyewe katika nyumba kufuatia limbikizo la madeni yaliyofichwa ya zaidi ya Pauni za Uingereza 150,000 na kuendelea kumficha mkewe kwa miongo mitatu, imeelezwa juzi.
Ibrahim Omar, mwenye miaka 57, mkazi wa Bolton huko Greater Manchester, aliweka picha za familia na vitu vingine binafsi katika gari la binti yake na kuacha funguo za gari nje ya nyumba yake kabla ya kujifungia na kujichoma moto ndani.
Keshia huyo wa zamani katika kituo cha mafuta alipata majeraha ya moto 'kwa kati ya asilimia 95 na 97' ya mwili wake wote na alitangazwa kwamba amefariki katika eneo la tukio, imeelezwa.
Alikuwa amemficha madeni yake, mkewe Mehrun kwa zaidi ya miaka 35, na watoto wao watatu, ilifahamika. Mikopo na kadi za fedha zinadhaniwa kuwa ni sababu nyuma ya madeni.
Mwili wa Ibrahim uligunduliwa na askari wa zimamoto mbele ya chumba chake cha kulala katika nyumba yake Agosti na uchunguzi wa mwili ulibaini kwamba alikuwa hai wakati moto huo ulipoanza.
Askari wa zimamoto, Anthony Wilkinson alisema mlipuko ulifunga mlango wa chumba cha kulala na kusukuma kuta za chumba nje. Alisema inaaminika ilikuwa 'kujitoa kafara' - kwamba Ibrahim alijichoma moto mwenyewe.
Alikuwa ni mwanaume mwenye kujali familia ambaye alikuwa mkuu wa kaya na alitaka kuitunza familia yake, taarifa iliyosomwa na ndugu zake ilisema.
Ibrahim alikuwa akisumbuliwa na mfadhaiko na alieleza kwa alikuwa na matatizo ya kukosa usingizi kutokana na hamu yake kuhusu pesa - lakini familia ya Ibrahim haikuwa na taarifa kuhusu uzito wa maradhi yake.
Kijana wake, Imran Omar alisema: "Imekuwa mshituko mkubwa kwa familia na jamii. Alikuwa maarufu sana, mcheshi na mwenye shauku. Alikuwa baba mwenye upendo na babu na tutamkumbuka milele."

No comments: