2012年3月1日星期四

CHEKA TARATIBU...

Kijana mmoja aliyepata ajira kwenye supermakert moja karipoti siku yake ya kwanza kazini. Meneja wake  kamsalimu kwa furaha na bashasha tele. Baada ya salamu meneja akamwambia, "Kazi yako ya kwanza itakuwa ni kufagia stoo yote." Yule kijana akajibu papo hapo, "Lakini mimi ni mhitimu wa Chuo Kikuu." Meneja akasema, "Oh, samahani sana. Nilikuwa sijajua hilo." Akaendelea, "Nipe hilo fagio, ntakuonyesha jinsi ya kufagia." Duh, balaa!!

没有评论: