TANESCO YAPATA HASARA SHILINGI MILIONI 50 KATIKA MIEZI MITATU...

Jengo la Makao Makuu ya Tanesco yaliyoko eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Shirika la Umeme (Tanesco) mkoani Mbeya limesema limepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 50 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Hatua hiyo inatokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa mafuta ya transfoma vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waadilifu kwa mali za umma.
Meneja wa Tanesco mkoani hapa, Simon Maganga amesema tangu kuanza kwa mwaka huu kumekuwa na tatizo la wizi wa mafuta  hayo ikilinganishwa na mwaka jana.
Maganga alisema wizi huo umekuwa ukifanyika sanjari na wizi wa
vipuri vingine katika transfoma jambo linaloipa hasara kubwa
shirika hilo.
Alitaja maeneo yaliyokithiri kwa wizi ni katika Wilaya ya Mbarali.  Kwa mujibu wake, Ofisi yake imepelekewa vifaa yakiwemo magari kwa ajili ya kusaidia kuendesha msako na kuwakamata wanaohujumu shirika.

No comments: