PAPA BENEDICT XVI AJIUZULU WADHIFA WAKE KANISA KATOLIKI...

Papa Benedict XVI akitangaza uamuzi wake huo mapema leo.

Habari zilizopatikana hivi punde zinasema, Baba Mtakatifu Benedict XVI ametangaza mapema leo kuachia ngazi nafasi yake kama kiongozi wa Kanisa Katoliki.
Katika uamuzi huo ambao umewashitua hata watu wake wa karibu, Baba Mtakatifu huyo mwenye miaka 85 alisema afya yake ilikuwa 'hairuhusu tena kuendelea na majukumu yake kutokana na umri wake kuzidi kuongezeka".
Alitangaza kujiuluzu kwake kwa lugha ya Kilatini katika mkutano wa makardinali wa Vatican leo asubuhi, akitilia mkazo kwamba kuongoza zaidi ya Wakatoliki bilioni duniani kote kunahitaji "vyote uimara wa akili na mwili."
Uamuzi wa Papa huyo haujawahi kutokea. Ni wa kwanza kujiuzulu tangu Gregory XII alipofanya hivyo mwaka 1415, lakini hakuna Baba Mtakatifu katika historia aliyewahi kujiuzulu kwa sababu za kiafya.
Ingawa maofisa walisema huko Vatican hakukuwa na shinikizo la yeye kujiuzulu, intaneti tayari imejaa na hisia kwamba kulikuwa na sababu zaidi za chuki nyuma ya uamuzi wake huo.
Akizungumza kwenye vyumba vya ikulu ya Vatican, Papa huyo leo aliwaambia makardinali: "Baada ya kuwa kupima dhamiri yangu kwa kurudia mbele za Mungu, nimemefikia uamuzi kwamba uwezo wangu wa kutokana na umri wangu mkubwa haukidhi tena kuendelea na majukumu kwenye taasisi hii.
Taarifa zaidi endelea kuperuzi ziro99blog.

No comments: