MWALIMU AGOMA KUWASAHIHISHIA WANAFUNZI KISA WAMETAJA BUNDUKI...

Mwalimu Dewey Christian (kushoto) aliyegoma kusahihisha kazi za wanafunzi wake wawili.
Mwalimu mmoja wa Kiingereza wa shule ya sekondari ya juu amegoma kutoa alama kwa kazi za wanafunzi wake wawili sababu tu walitaja bunduki.
Marshall Williams na Alex Wright, wanafunzi wa kidato cha juu katika Shule ya Sekondari ya Juu ya Denton iliyoko Dallas-Fort Worth, mjini Texas, walisema mwalimu huyo, Dewey Christian, aliwaandalia kazi ya kuandika ripoti kuhusu chochote walichokuwa wakitaka.
Marshall aliandika kuhusu safari aliyofanya kwenda kwenye maonyesho ya bunduki ya Fort Worth, wakati Alex aliandika kuhusu safari yake ya mawindoni, lakini wote wawili wamesema mitihani yao haikuelezea upigaji bunduki.
"Nilisema, 'Mimi na mama yangu tulikwenda kununua bunduki' na mara tu aliposikia neno bunduki aliniambia nikae chini," Alex aliieleza My Fox Dallas-Fort Worth.
Wavulana hao wote walielezwa wangepata sifuri kwenye kazi hiyo sababu ya mada hiyo na walikaripiwa mbele ya wenzao, chaneli hiyo ya habari iliripoti.
Baada ya Marshall kumweleza mama yake, Kimberly Williams, kuhusu kilichotokea, alikwenda shuleni kuonana na mwalimu huyo, na kurekodi muingiliano wao.
Kipande cha filamu kinaonesha Christian akielezea aligoma kutoa alama kwa kazi hizo sababu ya kuhusiana na vitendo vya hivi karibuni vya ufyatuaji risasi na vurugu katika mashule.
Lakini mama huyo alihoji kwamba ripoti ya kijana wake haikuhusisha rekodi zozote za siasa na kwamba hapo awali hawakuwa wameelezwa mada ipi hasa walikuwa wakiruhusiwa kuandika.
"Kama ilikwenda kinyume cha sera ya wilaya ningeunga mkono kabisa, lakini haikufanya hivyo," alisema. "Ni hisia zake binafsi juu ya kile anachoamini kinapenyezwa kwenye darasa lake na sikubaliani nacho."
Kijana wake aliongeza: "Nahisi kama amekanyaga uhuru wetu wa kujieleza. Alitueleza tusingeruhusiwa kujieleza na hakutaka hata kuzingatia tulichokuwa tumesema."

No comments: