MKANDARASI AFA KWA SHOTI YA UMEME AKIWA KAZINI...

Jengo lilipotokea tukio hilo Barabara ya Calverley.
Mkandarasi amefariki baada ya kupigwa shoti na umeme kwenye jengo la Marks & Spencer jana.
Phillip Dodd alikumbwa na janga hilo kwenye eneo la maduka la Royal Victoria Place huko Turnbridge Wells, mjini Kent.
Familia ya mgane huyo mwenye miaka 62 anayetokea Horley, Surrey, imeshataarifiwa kuhusu kifo hicho, polisi imesema.
Msemaji wa M&S alithibitisha kwamba janga hilo kweli limetokea.
Alisema: "Kulikuwa na tukio la ajali kwenye jengo hilo leo (jana) na tunapenda kuwapa pole familia ya marehemu.
"Kwa sasa tunafanyaa kila tuwezalo kusaidia huduma za dharura katika uchunguzi wao na kwamba hatuwezi kuzungumzia chochote zaidi katika hatua hii."
Polisi wa Kent walisema kifo hicho kinachukuliwa kama ajali kazini wakati maofisa wakifanyia kazi kujua mazingira yote ya kilichotokea.
Msemaji alisema: "Tuliitwa kabla ya Saa 9:30 mchana kwenye jengo hilo lililoko katika Barabara ya Calverley.
"Inaaminika mtu huyo alipigwa shoti ya umeme. Alithibitishwa kufariki eneo la tukio.
"Gari la wagonjwa lilifika na Wakuu wa Afya na Usalama wanachunguza tukio hilo.
"Kwa sasa inachukuliwa kama ajali nyingine tu hadi hapo uchunguzi kamili utakapokamilika."
Jengo hilo halikufungwa kutokana na ukweli kwamba eneo tukio lilipotokea si upande wa duka ambao una mkusanyiko wa watu, alisema msemaji huyo.

No comments: