CHEKA TARATIBU...

Padri kaingia kwenye baa na kuanza kuwahoji watu aliowakuta mle ndani., "Unataka kwenda mbinguni?" Mtu wa kwanza akajibu, "Ndio Fadha!" Padri akasema, "Simama pale ukutani." Kisha akamfuata wa pili na kumuuliza, "Unataka kwenda mbinguni? Yule mtu akajibu, "Bila shaka Padri." Padri akasema, "Simama pale ukutani." Akamfuata jamaa wa tatu na kumuuliza, "Unataka kwenda mbinguni?" Yule jamaa akajibu, "Hapana, sitaki." Padri kwa mshangao akasema, "Siamini hata kidogo. Unamaanisha kwamba ukifa hutaki kwenda mbinguni?" Jamaa akajibu kwa unyenyekevu, "Ooh, nitakapokufa, sawa. Nilidhani unatukusanya ili tuanze safari sasa hivi!" Duh…

No comments: