CHEKA TARATIBU...

Osama bin Laden kafariki na kwenda moja kwa moja kwenye lango kuu la mbinguni na kubisha hodi. Mtume Petro akajibu kwa sauti, "Nani?" Osama akajibu, "Ni mimi Osama." Mtume Petro akauliza, "Ni mambo gani mabaya unadhani umefanya duniani?" Osama akafikiri kidogo kisha akajibu, "Nilivuta bangi, lakini hutakiwi kunihukumu sababu sikufikisha moshi kwenye mapafu. Na niliua watu, lakini si kwa mikono yangu." Baada ya muda mfupi Mtume Petro akajibu, "Sawa, tumekubaliana hivi. Tutakupeleka mahali fulani pana joto sana, lakini hatusemi 'motoni.' Utakaa hapo kwa muda usiojulikana, lakini hatusemi 'milele.' Na 'usipoteze matumaini yote' uingiapo, wala usijizuie kupumua ukingojea kupoe." Kasheshe...

No comments: