KUSHOTO: Heather kabla ya kuingia katika Uislamu. KULIA: Heather akiwa na watoto wake. |
Kusilimu kwake kutoka msichana wa Ibiza hadi kuwa Muislamu wa kuvaa hijab ndani ya kipindi cha miezi mitatu kunaweza kuibua mshangao, na anakiri kwamba rafiki zake wanaweza kudhani ni moja ya kufifia kwake.
Lakini mwalimu aliye mafunzoni Heather Matthews mwenye miaka 27, anasema Uislamu umemletea 'upendo na furaha' ambayo hakuweza kuipata katika maisha yake ya zamani.
Heather, mama wa watoto wawili, alijiunga kwenye imani hiyo mpya wiki nne zilizopita, miezi miwili baada ya kurejea kutoka mapumzikoni huko Ibiza. Na anasema kwamba picha zake za zamani zilizopigwa katika safari hiyo zinaonesha yote yaliyo mabaya pamoja na picha cha urembo za Magharibi.
Alisema: "Nilifikiri nilihitaji kuchukua hatua na kuvaa katika njia nitakayojihisi vizuri mwenyewe. Naona wasichana sasa na kufikiri kuhusu taswira gani wanayoonesha kwa watu wengine, hasa wanaume.
"Ni juu ya kujiheshimu mwenyewe. Kama unavaa na kujiweka katika njia fulani, kisahihi au kimakosa, utachukuliwa katika njia hiyo hiyo.
"Uislamu umenifundisha kuhusu upendo halisi, si hamaki na tamaa. Ninaweza pia kuona maana katika ndoa iliyopangiliwa."
Uchunguzi uliofanywa na kundi la imani zaidi la Faith Matters umegundua idadi ya Waislamu waliosilimu nchini Uingereza sasa imevuka 100,000, ikiwa ni mara mbili zaidi katika kipindi cha miaka kumi.
Ripoti imekadiria karibu ya theluthi mbili ya watu wapya waliosilimu kuwa ni wanawake, wakiwa na wastani wa umri wa miaka 27 kama alivyo Heather.
Safari yake katika kusilimu ilianzia pale alipojaribu kumshawishi mumewe wa zamani Jerrome, ambaye alihamia Uislamu, kwamba dini hiyo haikuwa sahihi. Alikuwa 'na mashaka mno' kuhusu imani hiyo, na kuanza kusoma kuhusu dini hiyo ili kuzipa nguvu hoja zake.
Ingawa walikuja kutengana mwaka jana, aliendelea kujifunza kuhusu Uislamu, na kujitambulisha zaidi na zaidi kuhusu hilo. Kisha, wiki nne zilizopita, alimaliza mchakato wa 'kurejea'. Alisema: "Nilipitia maadhimisho ya 'Shahadah' ya kusilimu kuwa Muislamu kwa kurudia azimio la imani mbele ya Imam katika kituo cha kukuza imani kilichopo karibu na eneo langu.
"Nilikuwa na dada zangu kashaa wa Kiislamu pamoja nami na walininunulia hijab na vitabu vya Kiislamu kusherehekea. Ilishangaza sana."
Lakini anakiri kwamba marafiki zake wamepatwa na mshituko kwa kusilimu kwake katika dini ambayo inaaminika kuwa inawakandamiza wanawake.
"Watu wamekuwa wakijiuliza "Oh, hii ni hatua nyingine katika kufifia kwa Heather". Si kweli. Ni kile nilichokuwa nikitafuta katika kipindi chote nilichokuwa nikijaza maisha yangu kwa shauku ya kupanua maarifa," alisema.
Heather, mkazi wa Preston, amekuwa akikabiliana na wakati mgumu kutoka kwa familia yake. Lakini ni msukumo kutoka kwa wapitanjia kwamba ameshangaza sana hasa muonekano wa ushungi wake kichwani.
"Hakuna wanaume wanaojaribu kunitongoza. Ni ujingwa wa kuchukiza. Pale ninapovaa ushungi ninaweza kucheka na watu bila wao kufikiri ni kujitongozesha," alisema.
"Nimekubaliana kabisa na taratibu za Kiislamu kwa kutofanya mapenzi na mtu ambaye hujafunga naye ndoa na kulinda urembo wako kwa mumeo. Hivyo nafikiri mpenzi wangu ajaye atatakiwa kuwa aliyejifunza Uislamu ili kuelewa.
"Ni rahisi kwangu sasa kusema haya, kwa jicho pembe, kuwa nilifanya makosa, lakini nafikiri nilipotezwa na marafiki ambao wazazi wangu walidhani wananifaa, kujifunza kuwapenda kupitia kwanza urafiki."
Heather ameacha kabisa pombe, huku akikazania mlo unaoruhusiwa na imani hiyo na amepanga kufunga mwezi wa Ramadhani. Anacho kitabu cha Qur'an kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambacho anakisoma kila siku, na anataka kujifunza Kiarabu ili kuweza kuswali sala mara tano kwa siku.
Lakini amesema hatalazimisha Uislamu kwa binti zake wawili - Ellah mwenye miaka mitano na Halle mwenye miaka miwili, aliozaa katika ndoa yake na Jerrome.
"Watu wanafikiri nitakandamizwa lakini niko imara, najiamini na mwanamke huru," alisema. "Najua mimi ni mmoja wa watu ambao hawakufikiriwa kuingia katika Uislamu.
"Inanishangaza. Lakini nimefanya kwa upendo na furaha na imebadili kabisa maisha yangu."

No comments:
Post a Comment